Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya, ameagiza wahasibu wa Chuo cha Ualimu Moshi pamoja na Wakala wa Benki ya CRDB Wilayani humo, kukamatwa mara baada ya kugundua ubadhilifu wa shilingi milioni 78 zilizokuwa zinalalamikiwa na Wanafunzi Chuoni hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari DC Sabaya amesema kuwa mara baada ya kukutana na wote waliotajwa kuhusika na upotevu wa pesa hizo ikiwemo Bodi ya Shule, benki ya CRDB pamoja na Mawakala wa ELCT SACCOS, aliagiza wakae pamoja ili kubaini na kujiridhisha kiasi halali kilichopotea.
“Tumekubaliana kwamba wahusika wa wizi huo, huyu Muhasibu wa Chuo na yule Wakala watawajibika kulipa hicho kiasi kilichopotea”.
“kwa sababu nao watakuwa sehemu ya uchunguzi huo, lakini ili wasiharibu uchunguzi, nimeagiza wote wakamatwe kwa hiyo wote wawili wako ndani mpaka kesho saa 5:00 Asubuhi, watanipa majibu ya kilichofikiwa na tutaamua namna ya ulipaji wa fedha hizo ili Wanafunzi waendelee kubaki hapo Shuleni” amesema DC Sabaya.
Wanafunzi wa Chuo hicho waliandamana siku ya Jumatatu ya Septemba 9 na kushinikiza Serikali kuingilia kati sakata la utapeli wa zaidi ya Sh.milioni 78 za malipo ya ada ambazo hazionekani kwenye akaunti ya Chuo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai