Diwani kata ya Kia wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro Tehera Mollel, ameipongeza Serikali kwa juhudi kubwa inazoendelea kuzichukua katika kuboresha miundombinu ya barabara ndani ya kata hiyo, na kwamba hatua hiyo itachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi
Akizungumza katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai februari 6,2026 wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa robo ya pili ya mwaka 2025, inayoanzia octoba hadi mwezi disemba.
Hata hivyo diwani Mollel amesema Kata ya Kia inatarajiwa kunufaika na ujenzi wa barabara zenye jumla ya urefu wa kilomita 24, na kwamba barabara hizo kuwa ni Barabara ya Tindigani–Mtakuja yenye urefu wa kilomita 9 pamoja na Barabara ya Somali–Tindigani yenye urefu wa kilomita 15.
Pia Mollel ameeleza kuwa ujenzi wa barabara hizo ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha maisha ya wananchi, hususani waishio maeneo ya vijijini, kwa kuwezesha usafiri, biashara na upatikanaji wa huduma za kijamii.
Hata hivyo, pamoja na kuishukuru Serikali kwa utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo, Diwani huyo amewataka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuharakisha mchakato wa kuunganisha umeme katika kata hiyo, akisisitiza kuwa wananchi wa Kia wanasubiri kwa hamu kubwa huduma hiyo muhimu.
Ameongeza kuwa upatikanaji wa umeme utaongeza fursa za kiuchumi, kuboresha huduma za afya na elimu, pamoja na kuinua kipato cha wananchi kwa ujumla.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai