Diwani wa kata ya Masama Kati Kandata Kimaro amesema kukamilika kwa maabara mbili ya kemia na bailojia katika shule ya sekondari Lemira kumekuwa chachu ya wanafunzi kupenda masomo ya sayansi kwa kuwa wanajifunza kwa vitendo zaidi.
Mheshimiwa Kimaro amesema hayo wakati wa ziara ya kamati ya fedha ,uongozi na mipango ilipofika katika shule hiyo kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa maabara mbili ya kemia na baolojia iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni sitini hadi kukamilika kwake.
Amesema kuwa hapo awali wanafunzi walikuwa wanajifunza sayansi kwa nadharia pekee hali iliyokuwa ikiwakatisha tamaa huku idadi ya wanafunzi hao ikiwa ndogo, ambapo kwa sasa idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi imeongezeka kutokana na kukamilika kwa maabara hizo.
Hata hivyo Kimaro ameiomba halmashauri iweze kuwapatia fedha kwa ajili ya kuweka uzio katika eneo linalozunguka shule hiyo kwa ajili ya usalama wa wanafunzi kwani wapo baadhi ya wanafunzi wanaolala shuleni hapo.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mkuu wa shule hiyo Philipo Sekeyani amesema kuwa mradi huo umefanyika kwa kushirikiana na nguvu ya wananchi wa eneo hilo ambao wamefanya kazi ya kujaza udongo wakati wa ujenzi wa msingi hali iliyochochea mafundi kuendelea na kazi ya ujenzi kwa uraisi na kuharakisha ukamilishaji wake.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai