Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Hai wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kufuata sheria na kuzitambua stahiki zao kama haki yao ya msingi pindi wawapo kazini
Hayo yamesemwa na Afisa Utumishi Mkuu Mkoa wa Kilimanjaro Amosi Machirika akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdini Babu katika ufunguzi wa semina ya Madiwani yenye lengo la kuwajulisha majuku,mipaka Na stahiki zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai ndugu Edmundi Rutaraka amesema Baraza la miaka mitano iliyopita lilikua ni Baraza lenye uadilifu mkubwa kutokana na mafunzo waliyopewa hususani namna ya matumizi Bora ya fedha na mapato hivyo amesema mara baada ya mafunzo hayo ya siku mbili wataendelea kuwa na usimamizi mzuri katika kazi.
Nae Mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo ambaye ni diwani wa kata ya bomangombe ndg Evodi Njau ameeleza namna ambavyo mafunzo hayo yameonekana kuwajenga ikiwa ni pamoja
Mafunzo hayo yameonyesha matokeo chanya Kwa miaka mitano iliyopita hivyo yametajwa kuleta mafanikio makubwa katika miaka
mitano ijayo,
Kwa upande wake Mwenyeki wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Hai, Manguba Maganda ameeleza umuhimu wa mafunzo hayo huku akiwataka madiwani hao kuzingatia kile watakachofundishwa kama nyenzo katika utendaji waoo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai