Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai ole Sabaya ameagiza kupewa taarifa ya kamati inayodaiwa kufanya uchunguzi wa tuhuma za mkuu wa shule ya sekondari Lyamungo iliyosababisha mwalimu huyo kuhamishwa kituo cha kazi na kutaka TAKUKURU kufanya uchunguzi kubaini kama Kuna hila juu ya uhamisho huo.
Ametoa agizo hilo baada ya Mkuu huyo kudaiwa kupokea barua ya uhamisho na kutakiwa kuripoti katika shule ya sekondari Lemira baada ya kuwepo madai ya mwalimu huyo kutokuwa na ushirikiano na walimu wenzake.
Sabaya amemtaka afisa elimu kumpatia taarifa ya uchunguzi wa tuhuma zinazodaiwa kusababisha mkuu huyo wa shule ya secondari Lyamungo kuhamishwa, kwakuwa mwalimu huyo hakupewa nafasi ya kusikilizwa kwenye tuhuma anazotuhumiwa.
Amesema tangu mwalimu huyo kuwasili shuleni hapo mwezi August mwaka Jana amefanikiwa kumaliza migogoro shuleni hapo na kushtushwa na kitendo cha yeye kuhamishwa kwa tuhuma bila ya kusikilizwa.
Kwa upande wake afisa elimu secondari wilaya ya Hai Julius Kakyama amesema hajui chochote kuhusu tuhuma hizo, na kwamba uhamisho huo umetoka ngazi ya Mkoa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai