Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Edmund Rutaraka amewataka wasimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilaya ya Hai kuhakikisha wanawashirikisha wananchi katika utekelezaji wa miradi hiyo ili kurahisisha utekelezaji wake.
Ametoa maagizo hayo leo Januari 28 wakati kamati ya fedha,Uongozi na Mipango iliptembelea na kukagua Ujenzi wa maabara Katika Shule ya Sekondari Mukwasa.
Rutaraka amesema Wananchi wanaposhirikishwa Katika Miradi hiyo kunawezesha Wananchi kushiriki vema pale inapohitajika nguvu kazi.
Naye Diwani wa Kata ya Masama Kusini Cedrick Pangani ameishukuru Serikali Kwa kuendelea kuimarisha mioundo mbinu ya elimu.
Awali akisoma taarifa ya Ujenzi wa maabara hiyo,Mkuu wa Shule hiyo amesema Shule hiyo ilipokea milioni 30 Kwa ajili ya ukamilishaji wa maaba ya kemia na kwamba kazi zilizopangwa kufanyika zimekamilka.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai