Diwani Kata ya Romu Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro Salim Mfoy, ameishukuru Serikali kwa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo katika shule ya msingi Tolu.
Mfoy amebainisha hayo februari 6,2026 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Hai wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa robo ya pili ya mwaka 2025 inayoanzia oktoba hadi mwezi disemba.
Aidha Mfoy amesema majengo hayo yamegharimu kiasi cha Shilingi 80,600,000 na yamemalizika kwa asilimia 100.
Hata hivyo diwani Mfoy ameiomba serikali kuendelea na ujenzi wa nyumba ya walimu, ili kuweka mazingira rafiki ya kufundishia na kuongeza ufanisi na utendaji kazi kwa walimu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai