Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amewataka baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaokwamisha zoezi la kuwaandikisha wananchi katika daftari la orodha ya wapiga kura kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi ya kupiga kura.
Akizungmza na wanachi katika eneo la soko la Bomang’ombe hii leo, amesema wamejitokeza baadhi ya viongozi wa siasa wanaovuruga zoezi hili kwa kuwahamasisha wananchi kutojiandikisha na kwamba hatamvumilia kiongozi yoyote atakayeendelea kuvuruga zoezi hili muhimu kwa taifa.
“Walipogundua nyie wananchi mmepata mwamko, leo mnajiandikisha tumetoka asilimia nne hadi sasa tupo asilimia 66 wakaa juzi kuweka mikakati ya kukwamisha wanaanza kuwatisha eti wale watakaojiandikisha mtafaamiana nao, mnawatisha wananchi ninyi ni nani?”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai