Wanachi wilayani Hai wametakiwa kuhifadhi chakula kwa ajili ya matumizi ya familia ili kuzuia tatizo linaloweza kujitokeza la kukosa cha kwa baadhi ya jamii.
Rai hiyo imetolwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo wakati akizungumza na wakati akizungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho katika kata ya Bomang’ombe leo tarehe 02/08/2022 na kuwataka kutotumia mazao ya chakula kutengenezea pombe za kienyeji.
Amesema mwaka huu umekuwa na changamoto ya ukame jambo ambalo limeadhiri mavuno na kuwataka wanachi kuhakikisha wanatunza chakula walichokipata.
Amewataka pia wafugaji kuuza baadhi ya mifugo yao kipindi hiki ambacho bado ina hali nzuri ili fedha watakazo pata wanunue chakula na kukihifadhi ndani kwa matumzi ya baadae.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai