Afisa tawala wilaya ya Hai Mary Mnyawi amewataka wafanyakazi wilayani humo kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kutekeleza majukumu kwa ufanisi ili kuwa na haki ya kudai haki zao kwa waajiri ili na wao waweze kutimiza majukumu yao.
Akizungumza katika kikao cha baraza la wafanyakazi katika ukumbi wa halmashauri hiyo, Mnyawi ametaka vikao vya baraza la wafanya kazi kuwa yenye tija ambayo italeta ufanisi katika utekelezaji unaoleta matokeo chanya na siyo kuishia kwenye vikao pekee.
“Mwenyekiti wa baraza ndiye mwajiri kwa hiyo mtumishi anapofanya jambo ambalo lipo kinyume na utaratibu mwajiri ndiyo anapaswa kumchukulia hatua za kinidhamu, kwahiyo baraza hili linawajibu wa kufanya kazi yake hususani katika kurekebisha watumishi wanaokosea kabla halijafika kwa mwajiri lakini pia ni wajibu wetu kuenenda vizuri, kutekeleza majukumu yetu kwa wakati na kwa usahihi ili suala la hatua za kinidhamu lisitufikie”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai