Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano (TEHAMA)
Kitengo cha (TEHAMA) kimeanzishwa mwaka 2013 ambacho ni muunganiko wa Kitengo cha IT na Uhusiano. Kitengo hiki kinaongozwa na Sera ya TEHAMA (2003), na Sera ya Utangazaji Habari (2004). Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa 1) bila ya kuathiri sheria ya nchi, na kutafuta,kupata na kueneza au kusambaza habari na mawazo kupitia chombo cha habari chochote bila ya kujali mipaka ya taifa pia anayohaki na uhuru wa kutoingiliwa na mawasiliano (2) kila raia ana haki ya kupashwa habari wakati wote kuhusu matukio mbalimbali ya nchini na duniani kote yenye umuhimu kwa maisha na shughuli za wananchi , pia kwa masuala yenye umuhimu kwa jamii.
Majukumu ya Kitengo
Kuweka mahusiano bora baina ya Halmashauri pamoja na Umma na wadau mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa Umma.
Kuandaa machapisho mbalimbali ya Halmashauri.
kuratibu masuala ya kiitifaki ikiwemo kupokea wageni.
Usimamizi Wa Mifumo Ya Kompyuta(System Administration)
Usimamizi Wa Mtandao Wa Kompyuta pamoja Na Vifaa Vyake (Network And Hardware Adminstration).
Usimamizi Wa Benki Ya Takwimu(Database Administration)
Usimamizi wa tovuti na barua pepe (website administration & emails).
Kutekeleza sera ya TEHAMA na Serikali Mtandao.
Kuandaa mahitaji katika Ununuzi wa vifaa vya TEHAMA.
Kusimamia Kituo cha Redio ya Halmashauri
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai