Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Hai Yohana Sintoo amewataka wananchi katika jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka kuwaongoza kwa miaka mitano ijayo.
Sintoo ametoa wito huo katika kipindi cha Siku Mpya kinachorushwa na Redio Boma Hai alipokuwa anaelezea mwenendo wa shughuli za kampeni na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu kwenye jimbo hilo.
“Tuanze kuikumbuka tarehe 28 ya Oktoba mwaka huu; tuhamasike kila mmoja na kitambulisho chake tujitokeze kupiga kura kuchagua Rais, Mbunge na Madiwani” Amesema Sintoo.
Pamoja na kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura; Sintoo amewakumbusha wanasiasa, wanachama na wananchi wote kuzingatia maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya kumaliza shughuli za kampeni siku ya tarehe 27/10/2020 na kwamba siku ya kupiga kura hakutakuwa na kampeni wala kuvaa mavazi au kuonesha ishara za vyama kwenye eneo la kupigia kura.
Akizungumzia hali ya kampeni kwenye jimbo hilo; Sintoo amesema anawapongeza wadau wote vikiwemo vyama vya siasa kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa kuongoza shughuli za mikutano ya kampeni huku akiviasa vyama hivyo kufanya kampeni zao kwa kuzingtia ratiba iliyopo ili kuepusha migongano.
“Vyama vya siasa ni mdau muhimu wa uchaguzi ambao wana jukumu la kuhakikisha wanatunza amani wakati wa kampeni zinazoendelea kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha utulivu unakuwepo kwa sababu shughuli nyingine zinaendele na uchaguzi upite salama”
“Sisi kama tume, tutahakikisha kuwa tunasimamia sheria, kanuni na taratibu zote kwa ajili ya uchaguzi huu lakini pia nisisitize kwa vyombo vya habari kutoa habari ambazo zimenyooka kwani wananchi wakipewa habari za kupotosha italeta changamoto”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai