IDARA YA AFYA HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI.
Halmashauri ya wilaya ya Hai ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya vipatavyo 32 vya serikali katika mgawanyo wa Hospitali 1,vituo vya afya 4 na zahanati. Hospitali ya Mahame pia imeingia ubia na Halmashauri ili kusaidiana na vituo hivi katika kutoa huduma nafuu na nyingine za bure kwa makundi yaliyoainishwa na wizara. Huduma hizi zinafidiwa na serikali kwa zile ruzuku zinazopokelewa toka serikali kuu.
Idara ya Afya kama zilivyo idara nyingine za Halmashauri inatekeleza majukumu mbali mbali kulingana na sera na muundo wa Wizara ya Afya. Majukumu haya yanatekelezwa kulingana na ngazi tofauti za kiutawala zilizopo katika idara. Ngazi hizo za kiutawala ni kama ifuatavyo:
•Ngazi ya Utawala(CHMT)
•Ngazi ya Hospitali
•Ngazi ya Vituo vya Afya
•Ngazi ya Zahanati
•Ngazi ya jamii
MAJUKUMU YA NGAZI YA UTAWALA
•Kusimamia sera na miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya
•Kumshauri na kutolea ufafanuzi masuala yote ya kitaalam yanayohusu Idara ya Afya
•Kusimamia vituo vyote vya kutolea huduma za Afya ili vitoe huduma bora zinazoendana na viwango
•Kufanya ziara elekezi katika vituo vya kutolea huduma ili kutoa ushauri na kubaini changamoto mbali mbali zilizopo na kutafuta njia za kutatua changamoto hizo.
•Kupokea maagizo mbalimbali toka ngazi za juu na kuyafanyia kazi kasha kutoa mrejesho.
MAJUKUMU YA NGAZI YA HOSPITALI
•Kutoa huduma za wagonjwa wa nje
•Kuta huduma za maabara
•Kuta huduma za upasuaji mkubwa na mdogo
•Kutoa huduma za wagonjwa wa ndani
•Kutoa Huduma za Afya ya uzazi
•Huduma za kinga kwa magonjwa yanayoweza kukingwa
•Huduma za ustawi wa jamii zikiwemo huduma kwa wazee
• Kutoa huduma za Tiba,matunzo na Ushauri nasaha
•Kutoa huduma za vipimo vya mionzi (x ray na Ultrasound)
•Kutoa huduma za kuhifadhi miili ya marehemu (mortuary)
•Kutoa rufaa kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za kitaalam zaidi
NB. Hizi ni huduma zinazopatikana katika Hospitali yetu. Hata hivyo Halmashauri inaendelea kufanya upanuzi wa Hospitali ili huduma ziweze kuongezeka na zilizopo ziweze kuboreka zaidi.
MAJUKUMU YA NGAZI YA VITUO VYA AFYA.
•Kutoa huduma za wagonjwa wa nje
•Kuta huduma za maabara
•Kuta huduma za upasuaji mdogo na wa dharura kwa mama wajawazito
•Kutoa huduma za wagonjwa wa ndani
•Kutoa Huduma za Afya ya uzazi
•Huduma za kinga kwa magonjwa yanayoweza kukingwa
•Huduma za ustawi wa jamii zikiwemo huduma kwa wazee
• Kutoa huduma za Tiba,matunzo na Ushauri nasaha
•Kushiriki na wananchi katika kutekeleza shughuli za Afya
•Kutoa rufaa kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za kitaalam zaidi
NB. Hudma za upasuaji wa dharura kwa wajawazito bado hazijaanza kutolewa katika vituo vya Afya. Halmashauri kupitia vyanzo vyake mbalimbali imepanga kuweka miundombinu inayoweza kutoa huduma hiyo katika kila kituo cha Afya kwa awamu. Kito cha Afya Masama ndicho kitakachoaza kutekeleza mpango huu. Tunaalika wadau mbalimbali watakaoguswa kuchangia mpango huu unaotegemewa kutekelezwa kipindi cha 2017/18.
MAJUKUMU YA NGAZI YA ZAHANATI
•Kutoa huduma za wagonjwa wa nje
•Kuta huduma za maabara
•Kutoa Huduma za Afya ya uzazi
•Huduma za kinga kwa magonjwa yanayoweza kukingwa
•Kushiriki na wananchi katika kutekeleza shughuli za Afya
•Kutoa rufaa kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za kitaalam zaidi
MAJUKUMU YA NGAZI YA JAMII
•Kuhamasisha jamii katika masuala mbalimbali yanayohusu afya mfano chanjo,uzazi wa mpango,michango ya CHF.
•Uibuaji wa miradi mbalimbali ya afya katika ngazi ya jamii
•Kutoa taarifa za vifo vinavyotokea kwenye jamii.
AFYA
Wilaya ina vituo 64 vya kutolea huduma za Afya zikiwemo hospitali 2, moja inamilikiwa na serikali na nyingine inamilikiwa na shirika la dini (KKKT- Dayosisi ya Kaskazini),vituo 6 vya afya kati yake 5 vinamilikiwa na serikali na kimoja mtu binafsi. Zipo Zahanati 56 ambapo 27 zinamilikiwa na serikali, 18 mashirika ya Dini na 11 watu binafsi. . Katika kipindi cha mwaka 2017/2018 akina mama wajawazito waliohudhuria kliniki ya afya ya uzazi na mtoto ni 330% ya matarajio kutokana na kuboreshwa kwa huduma. Kiwango cha maambukizi ya VVU kwa wajawazito kilikuwa 1.5% na hali ya vifo vitokanavyo na uzazi katika kipindi cha mwaka 2017/2018 ni 1/100,000 Aidha, 92% ya akina mama wajawazito walipatiwa kinga dhidi ya malaria (IPT2).
Wilaya ya Hai imenunua dawa za kiasi cha shilingi 1,496,355,495.00 na kufanya kiwango cha upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 73.59 ya mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 90.57 mwaka 2018.
Tumejenga duka la dawa kwa gharama ya shilingi 41,485,900.00 linalotoa huduma kwa gharama nafuu saa 24 kwa wananchi pamoja na kukamilisha wodi ya wanawake katika hosptali ya wilaya kwa gharama ya shilingi 220,509,025.00.
Tumetoa elimu ya uzazi salama na kuleta ongezeko la wajawazito wanaojifungua kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 32.11% mwaka 2014 hadi 60.42% mwaka 2018 na kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka asimia 16% mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 4% mwaka 2018.
Hai ni miongoni mwa Wilaya chache zenye kituo jumuishi kinachotumika kutoa huduma kwa wananchi hasa watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia kinachofanya kazi kwa kushirikiana na Jeshi la polisi, daktari na ustawi wa jamii. Kwa mwaka 2015 hadi 2018 jumla ya kesi 22,368 zimeripotiwa na kushughulikiwa katika ofisi ustawi wa jamiii na watoto 2,128 wameunganishwa na familia zao.
Katika kutekeleza sera ya kuwajali na kuwahudumia wazee, wilaya yetu imewafikia wazee 4,199 waliopatiwa vitambulisho vinavyowasaidia kupata matibabu na zoezi linaendelea ili kuwafikia wazee wote wenye uhitaji.
USTAWI WA JAMII
Utafiti juu ya uelewa, ufahamu na mienendo ya watu na ulinzi kwa mtoto ulifanyika mwezi Mei 2010 kwa ushirikiano wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama Dar es salaam na shirika la kuhudumia watoto -UNICEF ilionesha kuwa, uelewa wa jamii juu ya masuala ya ulinzi kwa watoto ni mdogo, mfumo na miundo ya ulinzi kwa mtoto haikuwa imara katika kuwajibika kumlinda mtoto na kufanya idadi kubwa ya makao ya watoto yalioanzishwa kuwa chini ya viwango.
Kutokana na utafiti uliofanyika ziliundwa timu za ulinzi na usalama kwa watoto kuanzia ngazi ya Vijiji , Kata na Wilaya na zinafanya kazi kwa ushirikiano (networking) na ndizo zinazoibua matukio ya ukatili kwa watoto.
Jitihada hizi zilisaidia kupunguza idadi ya makao ya watoto kutoka 22 mpaka 4, ikijumuisha kuyafunga makao yanaoendesha huduma chini ya viwango na kutokuwa na usajili.
Elimu ya kupinga ukatili kwa watoto inaendelea kutolewa katika jamii kupitia Radio Boma Hai FM, Mikutano ya Vijiji, Taasisi za dini, shule za Msingi na Sekondari na imeleta mafanikio ya kuibua matukio mengi ya ukatili na kuripotiwa kutoka 59 mwaka 2010 hadi 6,077 mwaka 2018. Mafunzo yalitolewa kwa wazazi/walezi 311 juu ya malezi na unasihi ili kuwalinda watoto dhidi ya ukatili.
Pia ilisaidia kuunganisha watoto 403 kutoka makao ya watoto kwenda kwenye jamii (familia zao)na 738 waliopotea na wanaotoka mitaani.
Vilivile iliundwa /kutengenezwa Dawati la Jinsia na Watoto-Polisi wilaya ya Hai linalofanya kazi za kutetea na kulinda haki za watoto na kupambana na ukatili wa kijinsia (Gender Based Violence).
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai