KUANZA KWA IDARA:
Idara ya Elimu Sekondari katika Halmashauri ilianzishwa tarehe 1/7/2009 ilipong’atuliwa kutoka wizara ya elimu na utamaduni (kwa sasa wizara ya elimu sayansi na teknolojia).
IDADI YA SHULE NA WANAFUNZI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
MAJUKUMU YA IDARA
Idara ya Elimu ya Sekondari inatekeleza majukumu yake chini ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Sheria ya Elimu Na. 25 ya Mwaka 1978 na Marekebisho yake ya Mwaka 1995 na 2002. Pia zipo Kanuni, Nyaraka na Miongozo mbalimbali ya Serikali inayofafanua na kutoa mwelekeo wa kutekeleza majukumu ya Idara ili kufikia:
Dira ya Elimu na Mafunzo nchini ambayo ni “Kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa”.
Dhima yetu ambayo ni kuwa ni “kuinua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibu zitakazowezesha kupata idadi kubwa ya Watanzania walioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa letu”.
UONGOZI WA IDARA
Idara ya Elimu ya Sekondari inaongozwa na Viongozi wa Elimu wa aina tatu:
HALI YA MADAWATI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
Halmashauri ya Wilaya ya Hai hadi kufikia Desemba 2016 ilikuwa na madawati (Seti ya Kiti na Meza) 11512 sawa na idadi ya wanafunzi 11512 waliokuwepo katika shule za Serikali. Baada ya kuchaguliwa kwa jumla ya wanafunzi 4156 wa Kidato cha I – 2017, Halmashauri ilijikuta ikipungukiwa na jumla ya madawati 1945. Hii ni kutokana na tofauti ya Wanafunzi 2211 Waliohitimu Kidato cha Nne, 2016 na Kidato cha I – 2017 waliochaguliwa. Lakini hadi kufikia tarehe 23/02/2017, upungufu uliopo ni jumla ya madawati 783 kutokana na Idadi ya wanafunzi 2994 walioripoti.0.
Upungufu huo, tunakusudia kuupunguza kwa kugawa madawati mapya yaliyobaki ambayo ni zidio kwa ajili ya shule za msingi kwa sasa.
WATAHINIWA - CSEE 2016 |
WALIOFAULU (PSLE - 2016) KIDATO I - 2017 |
WALIORIPOTI HADI 23/02/2017 |
ASILIMIA ( % ) |
WALIOHAMA HADI 23/02/2017 |
WALIOHAMIA HADI 23/02/2017 |
WALIOJIUNGA PRIVATE HADI 23/02/2017 |
WASIORIPOTI HADI 23/02/2017 |
||||||||||||||
WAV |
WAS |
JML |
WAV |
WAS |
JML |
WAV |
WAS |
JML |
WAV |
WAS |
JML |
WAV |
WAS |
JML |
WAV |
WAS |
JML |
WAV |
WAS |
JML |
|
946 |
1265 |
2211 |
2019 |
2137 |
4156 |
1480 |
1514 |
2994 |
72.04 |
185 |
294 |
479 |
67 |
109 |
176 |
243 |
239 |
482 |
111 |
90 |
201 |
HALI YA UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI
Halmashauri ya Wilaya ya Hai kwa kushirikisha wadau na wananchi imejenga maabara katika shule za Serikali ambapo hatua iliyofikiwa ya vyumba vya maabara ni kama ifuatavyo: - Msingi 1, lenta/boma 12, Upauaji/ezekwa 27, Umaliziaji 14, na maabara zilizo kamili ni 33. Idara inaendelea kuhimiza ujenzi wa maabara sawa na nguvu na juhudi zilizoonekana awali hadi hatua iliyofikiwa. Idara inahimiza wananchi, viongozi wote ndani ya Wilaya kukamilisha maabara hizo:
idadi ya Shule |
Mahitaji |
Kamili |
Maendeleo ya Ujenzi |
||||
Msingi |
Boma/Linta |
Upauaji |
Umaliziaji |
Maelezo |
|||
29 |
87 |
33 |
1 |
12 |
27 |
14 |
Michango na mwamko wa wananchi ni hafifu |
Katika kusimamia elimu sekondari, serikali imetoa shilingi 3,924,623,751.79 kutekeleza elimu bila malipo, kuongeza nyumba za walimu kutoka 97 mwaka 2015 hadi 99 mwaka 2018 kwa kujenga nyumba mbili zenye uwezo wa kutumiwa na familia sita kila moja (six-in-one). Kuongeza vyumba vya madarasa kutoka vyumba 308 hadi vyumba 316, Halmashauri imeongeza matundu ya vyoo kutoka 456 mwaka 2015 hadi 478 mwaka 2018 na kuongeza maabara kutoka 6 hadi 25 kwa kutumia jumla ya shilingi 111,585,737.
Halmashauri yetu imepokea walimu wa masomo ya sayansi 22 na kuongeza idadi ya walimu kutoka 118 hadi walimu 140 katika juhudi za kuimarisha masomo ya sayansi shuleni. Walimu wamepata mafunzo mbalimbali ikiwemo walimu wa sayansi na lugha kufanya mafunzo mara nne yaliyogharamiwa na serikali kuu pamoja na semina ya kuboresha njia za ufundishaji.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai