UTANGULIZI.
Idara ya Usafi na Mazingira ni moja kati ya Idara zinazounda halmashauri ya Wilaya ya Hai. .Jukumu kubwa la Idara ni pamoja na usimamizi wa shughuli za Usafi na uhifadhi wa Mazingira kwa lengo la kudhibiti na kuzuia kuenea kwa magonjwa yatokanayo na uchafu na kudhibiti uharibifu wa Mazingira.Hii ni katika kuboresha ustawi wa jamii ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
KAZI ZA IDARA.
Halmashauri inapambana na uchafuzi wa mazingira kwa kutumia Sheria ndogo ya usafi wa mazingira pia elimu imeendelea kutolewa kwa jamii juu ya umuhimu wa usafi na utunzaji wa mazingira, kwa kupitia kamati za mazingira, vikundikazi vya mazingira, vikao vya WDC na vipindi maalumu vya Mazingira kupitia redio yetu ya Halmashauri Redio - Boma FM.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai