Majukumu ya Idara ya mifugo na uvuvi
Wilaya ina majosho 10 na vituo 10 vya afya ya Mifugo, kliniki 1 ya mifugo, vituo 20 vya kukusanyia maziwa, mnada 1 wa Mifugo na machinjio 1. Katika kuboresha lishe ya wananchi Wilaya ina mabwawa 53 ya samaki wa aina mbalimbali.
Idadi ya wafugaji waliopata mafunzo ya ufugaji bora imeongezeka kutoka 6,340 mwaka 2015 hadi 23,725 mwaka 2018, idadi ya mitamba iliyozalishwa na kusambazwa imeongezeka kutoka 477 mwaka 2015 hadi 2,234 mwaka 2018; idadi ya wafugaji waliopata elimu juu ya ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa imeongezeka kutoka 1,340 hadi 4,433. Vituo vya kukusanyia maziwa vimeongezeka kutoka 11 hadi 31. Jumla ya mifugo 256,529 imepatiwa chanjo ya kuzuia magonjwa. Wilaya imetekeleza agizo la serikali la kupiga chapa ng’ombe na kufanikiwa kwa asilimia 102% kwa kupiga chapa jumla ya ng’ombe 32,470.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai