Mkuu wa Mkoa wa Kilimnjaro Nurdin Babu ametoa pongezi kwa Mkuu wa wilaya ya Hai,Mkurugenzi pamoja na viongozi wengine kwa usimamizi bora walioufanya katika kusimamia miradi hiyo na anaamini itakamilika kwa wakati kama tarehe zinavyoeleza.
Ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo iliyofanyika Septemba 24/09/2025.
"Nimeridhika sana kuona usimamizi wenu mzuri kwenye wilaya ya Hai na matarajio yangu kwamba mimi nikiondoka nyie wenyewe mtakua mnapita mara kwa mara na kuhakikisha kwamba tarehe tulizokubaliana miradi hii inakamilika."
Pia amewakumbusha wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 kwakuwa ni haki ya msingi kwa kila mwananchi kumchagua kiongozi atakaeleta maendeleo.
Katika ziara hiyo Babu amekagua mradi wa madarasa,mabweni,nyumba pamoja na vyoo vya shule ya msingi Saashisha iliyopo kata ya Muungano, jengo la OPD kituo cha afya Masama kati,ujenzi wa madarasa na vyoo shule ya msingi Miaseni,ujenzi wa madarasa,mabweni na vyoo shule ya sekondari Kiselu,ujenzi wa madarasa na vyoo shule ya msingi Lambo,Ujenzi wa barabara pamoja na kituo cha utalii Chemka.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai