Kushughulikia mambo yote yanayohusu afya ya jamii, elimu na huduma za maji. Kamati hii pia itashughulikia mambo yanayohusiana na jitihada za wanannchi vijijini kujiletea maendeleo yao kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushauri, kushawishi, kuzindua, kuelimisha na kushirikisha wananchi hao hasa katika kutayarisha, kutekeleza, kusimamia na kutathmini mipango yao ya maendeleo.
Majukumu Maalum ya Kamati:
Kuandaa mipango madhubuti ya maendeleo ya upanuzi na ujenzi wa hospitali, vituo vya afya na zahanati
Kuandaa mipago ya maendeleo ya upanuzi na ujenzi wa shule za awali na msingi na elimu ya watu wazima kwa mujibu wa Sheria ya Elimu ya 1978 kama ilivyorekebishwa mwaka 1995.
Kupendekeza mipango ya ujenzi au upanuzi wa vituo,viwanja, majengo na mazingira ya burudani, starehe, mapumziko na michezo.
Kuamua juu ya mambo yanayohusu uhifadhi wa mambo ya kale na mandhari mbalimbali zenye sura nzuri.
Kuandaa na kuratibu njia bora juu ya uhifadhi wa nyaraka muhimu kwa ajili ya kumbukumbu hizo zitahifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa Sura ya 287.
Kpendekeza njia bora juu ya uhifadhi wa sanaa mbalimbali za ufundi na za maonyesho kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa Sura ya 287.
Kupendekeza namna ya malezi ya vijana ili waweze kuwa wazalishaji katika Taifa.
Kupendekeza namna ya malezi ya vijana ili waweze kuwa wazalishaji katika Taifa.
Kusimamia uanzishaji wa uendelezaji wa vikundi vya jamii na vya hiari vya wananchi katika Halmashauri kwa mujibu wa sera wa maendelo ya jamii.
Kusimamia na kuhakiki maeneo ya misitu, mapori, na mbuga zilizotengwa kama hifadhi ya mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Kupendekeza na kufanya tathmini ya uendelezaji wa mabonde, mito na mabwawa.
Kubuni na kupendekeza namna ya kidhibiti moto
Kubuni na kupendekeza mikakati ya utumiaji wa nishati mbadala, kuzuia ukataji miti ovyo, na kuhimiza upandaji miti kwa wingi.
Kuhakikisha kwamba ukaguzi wa majengo unafanyika mara kwa mara.
Kupendekeza mipango madhubuti ya ujenzi wa barabara vijijini na wilayani kwa ujumla.