TAARIFA YA IDARA YA KILIMO UMWAGILIAJI NA USHIRIKA
Ni mradi unatumia mtazamo wa shep katika kilimo cha Tanzania na mwishowe kutengeneza mtazamo unaoendana na mazingira halisi ya Tanzania. Shep ilianzia Japani na kwa bara la Africa ulijaribiwa Kenya 2006 ambako wakulima wadogowadogo wa Kenya walikuwa na chanagamoto nyingi na tayari wamepata ufumbuzi wa changamoto hizo ambapo kipato kimeongezeka, ujuzi na maarifa katika kulima vimeongezeka, kalenda ya kupanda na kuvuna inafuatwa na mabadiliko katika matumizi ya pembejeo. Mradi huu kwa sasa umesambaa katika nchi 10 za bara la Africa.
Mradi huu ni wa miaka mitano kuanzia Julai 2019 hadi Julai 2023. Katika kanda ya kaskazini mradi huu unatekelezwa katika mikoa ya Tanga wilaya ya Lushoto na Bumbuli, Kwa Kilimanjaro Hai na Moshi na Arusha wilaya za Meru na Karatu.
Kwa ngazi ya wilaya mradi umeanza Julay 2019 ambapo vikundi vilivyochaguliwa kutekeleza mradi ni kumi na moja (11) navyo ni Shamiri toka Kijiji cha Kawaya, Neema Envirocare cha Nshara, Umoja cha Mkombozi, Leira kijiji cha Rundugai, Tupendane kijiji cha Mkalama, Upendo na Amani vya kikavu chini, Orori kilimo kwanza na mwamko vya kijiji cha Orori, Wamboma cha shirinjoro na Mshikamano cha Kimashuku.
Usimamizi wa utekelezaji wa mradi huu unafanyika kwa ushirikianovwa wawakilishi wa JICA, Tamisemi, Wizara ya kilimo, Ofisi ya mkuu wa mkoa na na wawezeshaji sita wa ngazi ya wilaya.
Matokeo makubwa yanayotarajiwa kwa wakulima baada ya mradi kukamilika ni kama ifuatavyo;-
Kuwawezesha wakulima kulima kwa tija kwa kuwaunganisha na wadau mbalimbali ka ma taasisi za fedha na wauza pembejeo.
Kuwawezesha wakulima kuwa huru na kujiamini katika kulima na kuuza mazao yao.
Kujifunza kwa wakulima wengine na kuungana katika kuzalisha na kuuza ili waweze kutoka kwenye kulima na kuuza na kuelekea kwenye kilimo biashara kwa maana yakulima kwa ajili ya kuuza.
Wakulima watawezeshwa kumiliki kile wanachokifanya pia kuwa na mahusiano na wadau mbalimbali kwenye mnyororo wa thamani ili kujifunza kutoka kwao pamoja na kupata maarifa mapya.
2. KOROSHO
Zao la Korosho ni zao jipya kwa wilaya ya hai. Katika msimu wa Kilimo 2017/2018, Halmashauri ilipokea toka Bodi ya Korosho Tanzania jumla ya kilo 45 za mbegu za Korosho, kilo 25 za viriba (sheets), kilo 22 za matandazo, mwongozo na nakala ya mkataba wa kuzalisha miche. Kwa kuzingatia mwongozo, halmashauri iliteua Kikundi cha Mawoi Enviromental Care kusaini mkataba wa uzalishaji miche.
Uzalishaji na usambazaji wa miche
Kikundi hiki kilisaini mkataba wa kuzalisha miche 6,300 lakini kiliweza jumla ya miche 5,919 iliyosambazwa kwa wakulima. Kutokana na mwitikio na hamasa kubwa iliyokuwepo miongozni mwa wakulima , halmashauri iliweza kupata miche mingine 1,000 kutoka jeshi la Magereza - Karanga na kufanya idadi ya miche iliyosambazwa kwa wakulima kufikia 6,919. Halmashauri inakusudia kuzalisha na kusambaza angalau miche 10,500 kwa mwaka ambapo inahitaji jumla ya kilo 75 za mbegu za zao la Korosho kwa msimu wa 2020/2021 ili kuendeleza zao la Korosho.
Mafanikio
Changamoto
Pamoja na wakulima kuhamasika kulima zao la Korosho, kuna changamoto zinazowakabili kama ifuatavyo;-
Kilimo cha Vanilla Wilaya ya Hai kilianza mwaka 2000 kutokana na mafunzo yaliyotolewa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine Morogoro, lakini kutokana na kuyumba kwa soko la Vanilla, uzalishaji wake uliendelea kufifia hadi mwaka 2011 ambapo soko lake lilianza kuimarika na kufanya wakulima waanze tena Kilimo hicho. Wakulima walipata mafunzo ya uzalishaji kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu kupitia mashamba darasa 8. Pamoja na mafunzo hayo, Shirika hilo pia limewajengea wakulima kiwanda cha kusindika Vanilla pamoja na vituo 4 vya kukusanyia Vanilla katika vijiji vya Mudio, Nkwansira, Uswaa/Mamba na Kyuu. Pia Kampuni ya Natural Extract Industries (NEI) imekuwa ikitoa mafunzo ya uzalishaji, ukarabati wa mfereji, marando ya ruzuku na kuwaunganishia baadhi ya wakulima miundo mbinu ya umwagiliaji. Kwa sasa jumla ya wakulima takribani 1,535 wa wilaya ya Hai wanajihusisha na Kilimo hiki ambapo wanaendelea kupanua mashamba yao kila mwaka. Hadi sasa jumla ya miche takribani 22,810 ya Vanilla imeoteshwa sawa na hekta 34, uzalishaji wa sasa kwa mwaka ni Tani 1.4.
Halmashauri kupitia Idara ya Kilimo imeandaa andiko la mradi wa kuendeleza zao la vanilla ambapo ilipata TZS 16,000,000.00 kutoka benki ya NMB Kanda ya Kaskazini. Uhamasishaji ulioambatana na mafunzo ya Kilimo cha Vanilla umeshafanyika kwenye Kata 10 zenye jumla ya vijiji 43 ambapo lengo lilikuwa ni kutoa mafunzo kwa wakulima 30 kwenye kila Kijiji sawa na jumla ya wakulima 1,290.
Mwitikio wa wakulima umekuwa ni wa kuridhisha kwa baadhi ya maeneo na kwa sasa wanaandaa mashimo ya kuotesha Vanilla ambapo wanatarajiwa kupata miche ya Vanilla isiyopungua kwa bei ya ruzuku ya TZS 1,000 kwa mche. Ununuzi wa miche unafanyika kwa awamu ambapo kwa awamu ya kwanza jumla ya miche 2,800 yenye thamani ya TZS 7,000,000.00 imenunuliwa kutoka kikundi cha Mauki Vanilla Group na inatarajiwa kusambazwa kwa wakulima. Lengo kuu ni kununua na kusambaza miche 8,200 yenye thamani ya TZS 20,500,000.00, hii itawezekana kutokana na kutumia mfumo wa kusambaza miche kwa wakulima kwa bei ya ruzuku ya TZS 1,000 kwa mche. Aidha, Kikundi cha Mauki wanaendelea kuzalisha miche mingine ili iweze kununuliwa na kusambazwa kwa wakulima wakati wa msimu wa mvua za vuli.
Halmashuri imekuwa ikitoa mafunzo ya namna ya kudhibiti visumbufu vya mimea kupitia zahanati ya afya ya mimea. Wataalamu wa Idara ya kilimo kitengo cha mazao walipata mafunzo kutoka kwa madaktari wa mimea (Plant Doctors) kutoka Shirika la CABI international mwaka 2011 lenye makao makuu Uingereza. Wataalamu wamekuwa wakitoa elimu ya matumizi sahihi ya viuatilifu katika kudhibiti visumbufu kwenye mimea kwa kutambua madaraja ya sumu wakati wa matumizi kwa kuangalia rangi ya kidandiko cha sumu (Rangi nyekundu, Njano, bluu na Kijani) eneo lenye picha ya namna ya kujikinga wakati wa matumizi ya sumu husika. Lengo kuu ni kudhibiti madhara ya sumu iliyotumika kwenye mazao kumfikia mlaji.
Huduma za Zahanati ilikuwa inatolewa Siku za soko hasa soko la Mula, Kwasadala , Hai mjini na Rundugai, lakini kwa sasa huduma hii imesimama kwa kuwa wataalamu waliopata mafunzo ya namna ya kuendesha zahanati ya afya ya mimea kustaafu. Hivyo kwa sasa huduma hii imekuwa ikitolewa kwenye mashindano ya maonesho ya wakulima nane nane ambayo hufanyika Arusha kila mwaka kuanzia tarehe 1.08.2020 hadi 10.08.2020
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai