Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Sospeter Magonera, amewataka watumishi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanafanya vizuri katika mashindano ya michezo ya watumishi wa TAMISEMI SHIMISEMITA, yatakayofanyika mkoani Tanga kuanzia tarehe 15 hadi 30 Agosti mwaka huu.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kuaga timu ya watumishi wa Hai, iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Magonera amesema timu hiyo inabeba heshima ya wilaya nzima na hivyo inapaswa kupambana ili isishiriki tu, bali irejee nyumbani na ushindi.
> “Nendeni mkapambane, mkapige hatua na mkarejee Hai mkibeba medali za ushindi, maana nyinyi ndiyo sura ya Halmashauri yetu,” amesema Magonera.
Mashindano ya Shimisemita hukutanisha watumishi kutoka halmashauri mbalimbali nchini kwa michezo kama soka, mpira wa pete, mpira wa mikono, riadha na michezo mingine ya ushindani, yakiwa na lengo la kuimarisha mshikamano, afya, na ari ya utumishi wa umma.
Hai imejiandaa vizuri kwa mashindano haya, ikiwa na wachezaji wenye vipaji na ari ya ushindi, huku matumaini yakiwa makubwa ya kurejea nyumbani na ubingwa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai