FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA WILAYA YA HAI
Fursa nyingine ni uwekezaji katika shughuli za ufugaji ambapo vyama vya ushirika vinaweza kuanzisha mashamba ya ufugaji wa kisasa.
Uwekezaji katika kilimo cha maua
Yako maeneo ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji wa Hoteli za Kitalii hasa ukizingatia ni eneo lililo karibu na uwanja wa ndege wa Kimataifa (KIA).
Kuwekeza katika vivutio vya Kitalii
Aidha upo uwezekano mkubwa wa kuwekeza katika uhigadhi wa masuala ya kihistoria (makumbushio ya kihistoria).
Kuna fursa ya uwekezaji katika shule za ufundi na pia uwekezaji katika vyuo na vyuo vikuu.
Uwekezaji katika viwanja vya michezo na ujenzi wa vyuo vya michezo
Wilaya imegawanyika katika maeneo ya ukanda wa juu na ukanda wa chini (tambarare). Katika ukanda wa tambarare kuna upepo mwingi muda wote unaoweza kutumika kwa kuzalisha umeme kwa Teknolojia ya wind mill. Hii ni fursa nzuri ya uwekezaji katika Wilaya ya Hai.
FURSA YA UWEKEZAJI SEKTA YA MIFUGO
1. Ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa:
Kiwanda hiki kitawezesha kusinjdika maziwa yanayozalishwa na wakulima wadogowadogo, kitakuwa na uwezo pia waa kuhudumia Wilaya za jirani zikiwemo Siha, Meru, Simanjiro na Moshi Vijijini.
2. Kujenga machinjio ya kisasa:
Uchinjaji katika mazingira bora, utaimarisha afya za walaji kwa kuepusha magonjwa yanayotokana na mazingira machafu kuchina na kutunzia nyama.
Machinjio hii itakuwa na sehemu ya kuchinjia wanyama wakubwa na wadogo, pia kuku.
3. Uzalishaji wa majani yaliyokaushwa na kufungwa:
Uzalishaji unaweza kufanyika katika mashamba makubwa yaliyotaifishwa na kupewa vyamavya ushirika kuyaendesha. Majanii hayo yatahitajika sana katikaa kuzalisha mziwa kwa wafugai wadogo wa ng’ombe wa maziwa. Aidha yataweza kuuzwa katikaWilaya za jirani na kuongeza kipato kwa wakulima. Vile vil itawezesha upatikanaji wa ajira.
4. Kuanzisha vikundi vya kusindika na kutengeneza bidaa za ngozi.
FURSA ZA UWEKEZAJI - IDARA YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA
Waterfals/ Springs; Kijiji cha Nshara na Chemka.
Forest walking/ Pedestrian travel
Watching birds
Scenic beauty
Historical sites; Rebman tower at Machame, Churches, Mosques
FURSA ZILIZOPO KATIKA KITENGO CHA UTAMADUNI NA VIJANA
Halmashauri ina kiwanja kikubwa kinachoweza kupimwa viwanja vya michezo mingi. Kiwanja hiki kipo kwenye eneo lililopimwa na wananchi wamejenga nje ya kiwanja hicho – uwanja huu haujasawazishwa. Fursa hii tunaweza kuitumia kwa kujenga uwanja huo kwa kuzungushia ukuta kwa nje na tukawagawia watu maeneo ya kujenga vibanda vya Biashara ambavyo vinaweza kuingizia Halmashauri mapato. Pia watu wanataka kuingia kufanya mafano; mikutano, micchezo – watatoa kiingilio.
Tunalo eneo la kutosha kujenga kituo cha burudani – [Recreational centre] au kujenga kituo cha vijana cha kuonyesha sanaa zao siku za mwisho wa juma [weekends]
Eneo la ‘Green Belt’ lililopo kati ya TANESCO na majengo ya KNCU, tunaweza kutumia eneo hilo bila kuathiri uoto/mazingira ya eneo husika hatimaye tukapata sehemu ya kupumzikia watu baada ya kuzungushia uzio utakaosaidia kupaweka salama wakati wa matumizi.
Eneo hili linaweza kuingizia Halmashauri fedha nyingi kwani kila atakayeingia katika eneo hili atagharamia kwa kiingilio maalum kitakachowekwa na Halmashauri.
FURSA ZILIZOPO KATIKA IDARA YA ELIMU SEKONDARI
Kuanzisha Hosteli kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka mbali hasa wasichana.
FURSA ZA UWEKEZAJI SEKTA YA AFYA
Idara ya Afya inatoa huduma za Afya fursa zinazolengwa ni za kutna huduma za tiba (Curative Service), kuzuia magonjwa (Preventive service) na matunzo baada ya kupata madhara (Rehabilitative services).
Hadi sasa wilaya ina vituo vya huduma 60, kati ya hivyo 31 ni vya seerikali na 29 ni vya watu binafsi na mashirika ya dini.
Mahitaji ya watumishi wa afya ni makubwa, vipo vyuo viwili vya afya (TABIBU NA UUGUZI) vyenye uwezo wwa kudahiri wanafunzi 90. Hivyo upo uhitaji mkubwa wa vyuo vya afya kada ya maabara na famasia. Upo uhitaji mkubwa wa kituo cha kufanya uchunguzi wa magonjwa (Diagnostic centre) katika mji wa Bomangg’ombe ambapo kuna vituo Vinci hasa vya binafsi na hakuna huduma hiyo.
Hivyyo fursa za uwekezaji ni katika nyanja zifuatazo:-
STRENGTH: (Nguvu, Uwezo, Fursa)
WEAKNESS (Mapungufu)
CHANGAMOTO:
FURSA:
Upatikanajki mzuri wa maji safi na umeme.
FURSA ZILIZOPO IDARA YA FEDHA
(i) MLIMA KILIMANJARO
Watalii wengi wanaopanda mlima Kilimanjaro hupitia njia ya Machame.
Halmashauri ingetengeneza sheria ndogo ya kukusanya ushuru wa wageni wanaopanda mlima Kilimanjaro kupitia njia ya Machame ingejipatia fedha nyingi za kufanya maendeleo wilayani kwetu.
(ii) WAWEKEZAJI:
Ndani ya Wilaya ya Hai kuna wawekezaji wa aina nyingi, lakini hakuna sheria ndogo zinazo wabana kuchangia miradi ya Maendeleo. Sheria ndogo zitungwe kuwabana.
(iii) BODI ZA MAJI
Bodi zinazosimamia Miradi ya maji zinatakiwa zichangie fedha toka kwenye Ada za maji zitakazo tumika kulinda na kuendeleza vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla. Sheria ndogo inahitajika.
(iv) KUWEKEZA (INVESTMENT) (LGLB):
Halmashauri kwa kupitia mfuko wa Serikali za Mitaa na vyombo vingine vya fedha inaweza ikachukua mikopo na kuanzisha Miradi mbalimbali mikubwa ambayo itaipatia Halmashauri fedha ambazo zitawapatia wananchi wa Halmashauri huduma zinazohitajika.
TAARIFA YA MWAKA
MKOA WA KILIMANJARO
DETAILED DESCRIPTION OF SELECTED PARCHELS FOR THE LAND BANK IN KILIMANJARO REGION
NA |
H/W |
Eneo lilipo |
Ukubwa wa eneo |
Limepimwa/ Halijapimwa |
Mmiliki |
Miundombinu iliyopo |
Aina ya uwekezaji |
maelezo |
||
Maji
|
Umeme
|
Barabara
|
||||||||
2
|
Hai
|
Weruweru Industrial Area
|
4.80 acres
|
Limepimwa
|
M/S General Pharmaceutical 6000 Arusha.
|
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
Kiwanda
|
Linahitaji fidia au kutwaliwa.
|
|
|
Weruweru Industrial Area
|
4.60 acres
|
Limepimwa
|
M/S Njake Enterprises Ltd.
Box 13 Moshi |
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
Kiwanda
|
Linahitaji fidia au kutwaliwa.
|
|
|
Weruweru Industrial Area
|
4.60 acres
|
Limepimwa
|
M/S Nkibo Wood Lands Co. Ltd.
|
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
Kiwanda
|
Linahitaji fidia au kutwaliwa.
|
|
|
Weruweru Industrial Area
|
5.00 acres
|
Limepimwa
|
Onesmal Fanuel Mushio
|
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
Kiwanda
|
Linahitaji fidia au kutwaliwa.
|
|
|
Weruweru Industrial Area
|
5.00 acres
|
Limepimwa
|
M/S Lobo Investment Co.Ltd
Box 1636, Moshi. |
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
Kiwanda
|
Linahitaji fidia au kutwaliwa.
|
|
|
Weruweru Industrial Area
|
5.00 acres
|
Limepimwa
|
M/Elyi’s Co.Ltd. Box 8251, Moshi.
|
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
Kiwanda
|
Linahitaji fidia au kutwaliwa.
|
|
|
Weruweru Industrial Area
|
5.00 acres
|
Limepimwa
|
M/S Kibo Food Processing Ltd. Box 920, Moshi.
|
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
Kiwanda
|
Linahitaji fidia au kutwaliwa.
|
|
|
Weruweru Industrial Area
|
9.00 acres
|
Limepimwa
|
M/S Kilimanjaro Waters Ltd.
|
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
Kiwanda
|
Linahitaji fidia au kutwaliwa.
|
|
|
Weruweru Industrial Area
|
8.12 acres
|
Limepimwa
|
M/S Modson Garments Ltd. Box 290, Dar es salaam.
|
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
Kiwanda
|
Linahitaji fidia au kutwaliwa.
|
|
|
Weruweru Industrial Area
|
7.00 acres
|
Limepimwa
|
M/S S.A. Corporation Ltd. Box 372, Moshi
|
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
Kiwanda
|
Linahitaji fidia au kutwaliwa.
|
|
|
Weruweru Industrial Area
|
13.00 acres
|
Limepimwa
|
M/S Bonite Bottles Ltd. Box 1352, Moshi.
|
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
Kiwanda
|
Linahitaji fidia au kutwaliwa.
|
|
|
Weruweru Industrial Area
|
2.00 acres
|
Limepimwa
|
Kimashuku Commercial Centre, Box 15061, Dar es salaam.
|
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
Kiwanda
|
Linahitaji fidia au kutwaliwa.
|
|
|
Weruweru Industrial complex.
|
20 acres
|
Limepimwa
|
Mkurugenzi Mtendaji (W) Hai.
|
Yapo
|
Upo
|
Lami
|
|
|
|
|
Sanya Station
|
463 acres
|
Halijapimwa
|
EPZA
|
-
|
-
|
-
|
|
Upimaji na uthamini kwa ajili ya kulipa fidia kwa wamiliki wa asili bado haujafanywa.
|
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai