Wilaya ya hai imeadhimisha siku ya usafishaji kimataifa ambayo huadhimishwa kila ifikaspo jumamosi ya wiki ya tatu ya mwezi wa tisa,ambapo wananchi wamehimizwa kuzingatia usafi kwa kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka
Hayo yamebainishwa na kaimu mkuu udhibiti wa taka na usafi wa mazingira Alfred Njegite,alipokuwa akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya usafi katika mto sanya kuanzia katika daraja lililopo nyuma ya kanisa katoliki hadi daraja lililopo eneo la barabara kuu ya Moshi Arusha maeneo ya sheli ya mtoni wilayani Hai.
Ameeleza kuwa lengo la kufanya usafi katika eneo la mto huo ni kuweka mazingira ya mto huo katika hali ya usafi lakini pia kuwakumbusha wananchi kuwa eneo hilo si sehemu ya kutupa taka bali linapaswa kuwa safi kila wakati.
Naye Julius Sway mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Hai amesema kuwa zoezi la ufanyaji usafi katika mazingira yanayotuzunguka, yasisubiri kufanyiwa usafi wakati wa maadhimisho ya siku ya usafi, bali zoezi la usafi wa mazingira liwe desturi yetu kila wakati.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Uzunguni Andason Somi amewataka wakazi wa eneo hilo ambalo ndiko mto huo unapopita, kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kuepula kutupa taka katika mto huo,kwani endapo mwananchi yeyote atakayebainika akitupa taka katika mto huo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kulipa faini ya shilingi elfu hamsini.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai