Mkuu wa Wilaya ya Hai Hassan Bomboko ameagiza uchunguzi kufanyika kufuatia Darasa la awali katika Shule ya Nkronga iliyopo kata ya Masama Magharibi lililoungua na moto usiku wa kuamkia leo.
Katika ziara yake shuleni hapo mapema leo, Bomboko amevitaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa haraka juu ya sababu za kuungua kwa darasa hilo ambalo halisababisha madhara ya kibinadamu.
“vyombo vitaendelea kufanya kazi, kwa sasa watu wasiingie hadi taasisi husika itakapo kamilisha kazi yake hii ni kwa ajili ya usalama wa Wanafunzi, Waalimu na Wananchi wanaozunguka eneo hili kwakuwa hadi sasa hatujui moto huu umesababishwa na nini”amesema Bomboko.
Katika kushugulikia tatizo hilo amewataka viongozi wa shule na kata kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mamlaka husika ili kufanikisha zoezi kwa haraka.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Dionis Myinga amesisitiza umuhimu wa utoaji wa taarifa kwa wakati hasa kwa nyakati za dharura.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Melody Lema amesema baadhi ya vifaa vilivyokuwa katika darasa hilo vimeungua ikiwa ni pamoja na meza na zana za kufundishia na kwamba wanafunzi wa awali kwa sasa wanatumia darasa la saba.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai