Yapo maeneo makubwa 2 yenye hekta 515.6 yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji. Moja likiwa ni lililoainishwa takribani miaka 10 iliyopita kuwa ukanda wa uwekezaji kwa ajili ya EPZ. Hili liko kijiji cha Sanya Station na lina ukubwa wa hekta 463, halijapimwa wala kulipiwa fidia kwa mujibu wa sheria na hivyo kuendelea kuvamiwa na kuendelezwa. Pili ni eneo la Weruweru Industrial Complex lenye ukubwa wa hekta 52.6 ambalo limeshapimwa na viwanja kumilikishwa kwa wawekezaji mbalimbali.
Hata hivyo, wananchi wengi waliomilikishwa viwanja hivyo wameshindwa kuviendeleza kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu. Kutokana na hali hiyo, serikali tayari imetoa maelekezo ya kubatilisha milki husika ili viwanja vitolewe kwa wawekezaji wengine wenye uwezo wa kuviendeleza.
Halmashauri ikishirikiana na Serikali kuu inafanya mikakati shirikishi ya uanzishaji, uendeshaji na usimamizi wa viwanda pamoja na kufufua viwanda. Pia inatekeleza dhana ya uchumi wa viwanda kwa kuhamasisha sekta binafsi kufungua viwanda kama vile kiwanda cha mabati, (Northpole Company Ltd) kilichopo Mungushi, Kiwanda cha kuku wa mayai (Afro Farm Ltd) kiwanda cha kutengeneza vyombo vya plastiki (Ametech Plastic Group) kilichopo Hai mjini na kiwanda cha kutengeneza pombe ya ndizi (Jackro Investment) kilichopo Masama Rundugai.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai