WASILISHO KWA MKURUGENZI NA WATUMISHI WA HAI 12/10/2020
IDARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
Idara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ina jukumu la kusimamia shughuli zote za uzalishaji, Afya na usimamizi wa sheria za mifugo na uvuvi na pia kutoa tarifa mbali mbali za kisekta kwa wadau mbali mbali. Makao Makuu ya Idara ni katika Jengo la Kliniki ya Mifugo ya Wilaya lililopo karibu na Ofisi ya Idara ya maji
Rasilimali watu
Idara ya Mifugo na Uvuvi ina watumishi waajiriwa 27, kati yao watumishi 6 wanafanya kazi Makao makuu, 19 wapo katika Kata na Vijiji, 2 wanafanya kazi ya ukaguzi wa nyama katika machinjio ya wilaya. Pia kuna watumishi 13 wanaofanya kazi kwa kujitolea, kati yao 3 wapo makao makuu na 10 wanafanya kazi katika vijiji. Wataalamu 39 wa uhimilishaji wa ng’ombe wa maziwa ambao wanatoa huduma ya uhamilishaji baada ya kuwezeshwa ujuzi huo na Halmashauri kwa kushirikiana na vyama vya ushirika vya maziwa na wadau mbali mbali wa maendeleo katika sekta ya maziwa kama SNV, MATCH MAKER, ADGG na LAND ‘O LAKES.
Idadi ya mifugo katika wilaya ya Hai ni kama inavyoo nyeshwa kwenye Jedwali hapa chini
Ng’ombe wa Maziwa wa kisasa
Ng’ombe wa nyama wa kisasa Ng’ombe wa kienyeji. Mbuzi wa Maziwa Mbuzi wa Kienyeji Kondoo Kuku wa nyama (broilers) Kuku wa mayai Kuku wa kienyeji Bata Maji Bata Mzinga Bata Bukini Kanga Punda Nguruwe Ngamia Sungura Sili(Simbilisi)Guinea pigs Mbwa. Paka Farasi |
48,316
347 61,431 1,837. 67,001 34,357. 56,378. 124,452. 344,683 6,255. 237. 130. 428 1,562 36,820 120 6,547 421. 7,473. 1414 10 |
Uzalishaji wa bidhaa za mifugo
Ng`ombe wa Asili wanafugwa ukanda wa tambarare kwa njia ya ufugaji huria na wanazalisha wastani wa Kg 180 za nyama kwa ng’ombe 1 na wastani wa maziwa lita 3 kwa siku kwa ng’ombe 1, kwa upande wa mbuzi na kondoo wanazalisha Kg 10 hadi 15 za nyama kwa kila 1 na nguruwe wanazalisha Kg 70 hadi 120 kwa mnyama 1.
Ng’ombe wa kisasa wa maziwa wafugwao Ukanda wa Kati na wa Juu kwa njia ya ufugaji wa ndani (Zero Grazzing System) na huwa wanazalisha wastani wa lita 11.5 za maziwa kwa ng’ombe kwa siku moja ikiwa ni ongezeko la lita 4.5 ukilinganisha na uzalishaji wa lita 7.0 kwa ng’ombe kwa siku za mwaka 2018
Mtamba wa ng’ombe wa Maziwa aliyeshika nafasi ya pili ya ng’ombe bora wa maziwa kikanda maonyesho ya 88 Arusha mwaka 2019
Ng’ombe wanaokamuliwa kwa wastani ni 12,107 ambapo uzalishaji kwa siku ni lita 139,159.5 na kwa mwaka ni wastani wa lita milioni 50.8
Kuna vyama vya ushirika vya maziwa 16 vilivyosajiliwa pamoja na vikundi 8 vinavyojihusisha na biashara ya kukusanya na kuuza maziwa. Vyama vinne ambavyo ni Nronga, Kalali, Marukeni na Ng’uni vinasindika maziwa na kutoa mazao ya maziwa kama siagi, mtindi, Yoba na jibini.
Idara ya Mifugo kwa kushirikiana na Shirika la SNV tuliratibu na kushauri kuunganisha vyama 16 vya ushirika vya maziwa toka Halmashauri yetu na vyama vinne toka Wilaya ya Siha kuungana na kuunda Muungano wa vyama vya ushirika vya maziwa Mkoa wa Kilimanjaro vikijulikana kama (Kilimanjaro Dairy Co operative Joint Enterprises) kwa kifupi J.E. Kazi za umoja huu ni kuunganisha nyama vya ushirika wa maziwa katika kutafuta soko la pamoja la maziwa, kuwa na sauti moja katika biashara ya maziwa, kutafuta wawekezaji mbali mbali wa kuwekeza katika sekta ya maziwa, kutafuta na kusambaza pembejeo bora za mifugo ikiwemo malisho na vyakula vya ziada (Concentrates) .
Muungano wa J.E. kwa sasa umeingia makubaliano na kiwanda cha vyakula vya mifugo cha Harsho kwa oda maalum ya kuzalisha chakula bora cha ng’ombe wa maziwa na kukisambaza katika vyama vyote kwa bei nafuu.
Katika kuharakisha maendeleo kwenye sekta ya mifugo Idara inafanya kazi na wadau mbali mbali wa maendeleo ambao ni kama ifuatavyo:-
Shirika la Maendeleo la Uholanzi ( SNV). Shirika hili linasaidia katika kutoa mafunzo ya ufugaji bora kwa wafugaji, mashamba darasa ya malisho bora, usindikaji wa maziwa na kutafuta masoko. Pia wamewezesha kila kituo cha maziwa kuwa na TOT (Wakufunzi) ambao wamepata elimu ya kuzalisha maziwa yalio bora na huwa wanatoa elimu hiyo kwa wafugaji katika vikundi na shirika za maziwa, pia wamesaidia kufundisha vijana 11 juu ya Uhimilishaji wa ng’ombe wa maziwa AI na kuwawezesha vifaa vya kazi pamoja na usafiri, , kushiriki paredi ya ng`ombe wa mziwa Dodoma, kuwezesha unywaji wa maziwa mashuleni na kuwezesha vijana 10 wanaosafirisha maziwa kutoka sehemu za mbali na vituo vya maziwa.
Shirika la Match Maker Associates (MMA) Shirika hili limewezesha vikundi 6 vya vijana kufanya kazi kwenye mnyororo wa thamani wa maziwa kwa kuwapa elimu ya kusindika malisho na kuwapa mashine 6 za kusindika malisho kila moja ikiwa na thamani ya Tshs. 13 milioni na pia katika kuboresha biashara ya maziwa shirika limewezesha vikundi vitatu vya vijana kumiliki mashine za Milk ATM 3 moja ipo hapa Bomang`ombe , na mbili Moshi Mjini kila moja ikiwa na thamani ya Tshs. 16.5 milioni. Mashine hizi kwa sasa zinauza maziwa bora na salama kwa walaji muda wote.
Mashine ya kuchakata malisho ya Kikundi cha Vijana Kijiji cha Saawe
Mashine ya kuuza maziwa (Milk ATM)
Shirika la Capacity Bulding for Organizations (CABO). Shirika hili linatoa Elimu ya Uongozi katika Ushirika na kusaidia uhamasishaji wa uundwaji wa vikundi vya maziwa vijijini na kuwezesha kinamama na vijana walioko kwenye mnyororo wa thamani wa maziwa kuunganisha wafugaji na wauza pembejeo za mifugo kama vyakula, vifaa vya kukamua na kupima na kuhifadhi maziwa.
Taasisi ya Utafiti wa mifugo Tanzania (TALIRI) kupitia mradi wa Africa Dairy Genetic Gain (ADGG) kwa Ushirikiano na Halmashauri yetu tuliweza kufundisha wataalamu 10 elimu ya uhimilshaji wa ng’ombe wa maziwa na kuwanunulia vifaa vya kufanya kazi hiyo pamoja na usafiri wa piki piki na mitungi ya kuhifadhi mbegu za ngombe na pia tuliweza kupima Genetic Potantial za ng`ombe wa maziwa katika Wilaya yetu na kutuwezesha kushiriki maonyesho ya ng’ombe bora wa maziwa kitaifa yaliyofanyika Dadoma ambapo ng’ombe wote 6 kutoka Wilaya ya Hai walikuwa ng’ombe bora wa maziwa kati ya ng’ombe 40 walioshiriki maonyesho hayo.
Pia Taasisi imetoa Hereni zenye namba za utambuzi wa ngombe bora wa maziwa ili kuwezesha kuingizwa kwenye mfumo wa utambuzi wa ng’ombe bora kwa baadhi ya wafugaji.
Miundo mbinu iliyopo
Jengo la ofisi ya Idara ambalo pia ni kliniki ya mifugo ya Wilaya. Pamoja na shughuli za kiofisi tunafanya matibabu ya mifugo na upasuaji wa mizoga ili kutambua magonjwa ya mifugo na kutoa ushauri kwa wafugaji. Miundo mbinu mingine ni pamoja na Vituo vya mifugo 10, majosho 9, Mabirika ya kunywea maji 9. Vituo 26 vya uhimilishaji ng’ombe wa maziwa, mabucha 154 visima vya kuchinjia mifugo 122, machinjio 1. Idara kwa kushirikiana na wafugaji wa Kijiji cha Sanya Station tumehamasisha wafugaji na kufufua josho la Sanya Station na kwa sasa linafanya kazi.
Ng’ombe wakitoka kuoga Josho la Sanya Station.
Pia tumeshapata kibali cha kuanzisha mnada wa mifugo eneo la ekari 12 lililotengwa katika Kijiji cha Sanya Station. Eneo hilo limeshapimwa na ramani ya Ofisi na choo imeshakamilika. Mchakato wa fedha za ujenzi wa mnada huu unaendelea.
Magonjwa ya mifugo
Magonjwa makubwa yanayosumbua mifugo katika Halmashauri yetu ni Ndigana Baridi, na Ndigana kali.
Magonjwa ya Kiwele (Homa ya kiwele) , upungufu wa madini. Kimeta FMD, LSD, Rabies, NCD, Fowl pox, Fowl Typhoid, ASF . Wataalamu wanatoa tiba kwa magonjwa haya kila mara yanapojitokeza na pia kutoa chanjo kwa magonjwa ya mlipuko kwa kufuata ratiba za chanjo za mifugo.
Wataalamu wa Mifugo wakichunguza ugonjwa wa Homa ya Nguruwe Kijiji cha Nshara
Changamoto
Kwa kuwa maeneo ya kufugia ni madogo kuna changamoto kubwa ya kupata malisho ya kutosha kwa ajili ya kulisha mifugo. Wataalamu wamekuwa wakishauri wafugaji kuotesha malisho bora kama vile Majani ya Rhodes, Elephant grass, Guatemala grass, Desmodium, Lucern, Lukina, calliandra ambayo ni malisho bora na yanakua haraka na pia yanatoa mavuno mengi katika eneo dogo.
Uchakavu wa miundombinu ya machinjio na majosho ambapo inahitajika ukarabati mkubwa.
Ufugaji bora kwa watumishi
Ili kujikwamua na ugumu wa maisha Idara inashauri watumishi kufuga Kuku wa nyama na mayai kwa kuwa ni ufugaji rahisi na una faida ya kupata lishe na kuongeza kipato na pia hutumia nafasi ndogo. Zaidi madawa tiba na chanjo zipo zinapatikana, ramani za mabanda rahisi zipo na wataalamu tupo.
Ufugaji wa samaki wa kisasa
Huu ni ufugaji mwingine ambao ni rahisi na samaki aina ya kambale wanapatikana na wanakua haraka kwani wanaweza kufikia uzito wa Kg. 1 katika umri wa miezi minne.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai