Jamii imetakiwa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inaofanyika katika kata zao ikiwemo miradi ya elimu ili kuwezesha miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kuleta manufaa kwa jamii husika.
Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu ya watu wazima na Elimu Maalumu Emaculata Mgaza ambaye ni msimamizi wa Mradi wa Boost kwa shule ya Msingi Tolu iliyopo Kata ya Romu na Kambi ya Raha iliyopo Kata ya Muungano ambazo zimepewa 88,600,000 kwa kila mmoja.
Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mkuu wa Idara ya Msingi na Awali Jafari Zaidi amesema kuwa serikali imetoa fedha hizo kwa ajili ya kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika shule za awali na msingi.
Zaidi amewataka amewataka watekelezaji wa mradi huo kusimamia vema mradi huo ili lengo la serikali lifikiwe.
Nao baadhi ya wananchi wameipokea kwa furaha kubwa miradi hiyo ambapo wameeleza kuwa wanafunzi wataondokana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili ikiwa ni pamoja na msongamano katika madarasa pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai