Wananchi wa kijiji cha Kware wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha mbalimbali kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kijiji hicho.
Akitoa taarifa ya mapokezi ya fedha kiasi cha 49,000,000/= (Milioni arobaini na tisa laki nane) fedha ambazo zitatumika katika zahati ya kware, afisa mtendaji wa kijiji hicho Edwine Lamtey amesema kuwa fedha hiyo ni kwaajili ya mradi wa Usambazaji endelevu wa maji vijijini na usafi wa mazingira (Sustainable rural water supply and sanitation.)
Aidha pia amesema kuwa fedha hiyo itatumika kwaajili ya kuboresha miundo mbinu ya maji, vyoo, kichomea taka, shimo la kutupia kondo la nyuma pamoja na shimo la kutupa majivu.
"Tumepokea fedha hizi, kazi yangu mimi kama msimamizi wa hii miradi ni kuhakikisha inatekelezwa kama ilivyokusudiwa na serikali pamoja na kuhakikisha thamani ya fedha katika mradi ionekane na pia niwatake watumishi pamoja na wale mtakaoingia katika hizi kamati hii ni fedha ya serikali itatumika kwa malengo mahususi tu" Alisema Edwine Lamtey.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho mwenyekiti wa kijiji cha Kware Sabastian Kimaro amesema kuwa mbali na ujio wa fedha hiyo, hivi karibuni kijiji kilipokea milioni kumi kwaajili ya ununuzi wa madawati, Milion 3 fedha ya mfuko wa jimbo kwaajili ya ujenzi wa jiko ambao uko mbioni kukamilika.
"Pamoja na hizi nilizozitaja Kware sasa tumeamka na tunapambana kupata maendeleo ambayo hapo awali tuliyapoteza, Leo nini ni mashuhuda tunaenda kupaua ofisi yetu mpya na tayari vifaa vya upauzi tunavyo ambavyo ni wanachi wa kware wamejitoa na siri kubwa ni ushirikiano wa viongozi wa kijiji na wananchi" Alisema Mwenyekiti Kimaro.
Nae Sabrina Lema ambaye ni mwananchi wa kitongoji cha Boma Kati kilichopo kijijini hapo amesema kuwa kwa muda mfupi kumekuwa na maendeleo makubwa ikiwa ni muunganiko mzuri na ushirikiano kati ya wananchi, serikali ya kijiji pamoja na viongozi wa juu.
Katika mkutano huo pia wananchi wa kijiji hicho walipewa elimu ya urasimishaji wa ardhi ikiwa ni njia ya kuiongezea ardhi thamani pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi, zoezi ambalo litaanza hivi karibuni.
Kijiji cha Kware ni miongoni mwa vijiji vinne vilivyopo katika kata ya Masama Kusini ambapo kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi kijiji hicho kina idadi ya watu 1750 huku shughuli kubwa zikiwa ni kilimo, ufugaji pamoja na biashara.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai