• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Hai District Council
Hai District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Hai

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Utumishi
      • Ardhi na Maliasili
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Taarifa Idara ya Kilimo
      • Mifugo na Uvuvi
        • Wasilisho Mifugo
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Tehama na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
      • Maporomoko ya Maji ya Nshara
      • Chemchemi ya Chemka
      • Mila na Utamaduni
      • Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Industry and Trade
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Kilimo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Mipya
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
      • Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi
      • Ahadi ya Uadilifu Watumishi
      • Fomu ya Maombi ya Likizo
      • OPRAS Walimu
      • OPRAS Watumishi
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Taarifa kwa Umma-Mikopo
    • Jarida
  • Mifumo
    • Mfumo wa Kiuhasibu (FFARS)
    • Mfumo wa Bajeti (Planrep)
    • Mfumo wa Vibali Safari za Nje
    • Mfumo wa Taarifa za Mapato (LGRCD)
    • Mfumo wa Taarifa za Shule (TanzaniaSIS)
    • Usajili Kupata TIN (TRA)

Silinde Azindua Huduma Afya ya Kinywa na Meno Wilayani Hai

Imetumwa: February 11th, 2021

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais –Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa David Silinde (MB) amewataka wananchi kuondoa hofu zinazosababishwa na taarifa za uongo zinazosambazwa dhidi ya ugonjwa wa Corona ila wachukue tahadhali za msingi zitakazoimarisha afya zao.

Ameyasema hayo leo Februari 11 wakati wa ufunguzi wa jengo la huduma za kinywa na meno katika hospitali ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro lililojengwa kutokana na fedha za makusanyo ya mapato ya ndani.

Ameitaka jamii kuzingatia maelekezo ya Serikali hasa yanayotolewa na Rais John Magufuli kuwa ugonjwa wa Corona unatibika kwa nguvu za Mwenyezi Mungu na kutumia dawa lishe kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya.

Aidha Naibu Waziri Silinde amezitaka halmashauri nyingine nchini kuiga mfano wa halmashauri ya Hai kwa kutekeleza miradi ya maendeleo yenye tija kwa wananchi kwa kutumia vyanzo vya fedha za mapato ya ndani badala ya kusubiri kila kitu kifanywe na serikali kuu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ametumia uzinduzi huo kuwatoa hofu wananchi kuhusu  maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa kuwataka wasiogope kufanya shughuli zao za maendeleo kama ilivyo desturi na kujitafutia kipato chao na familia zao kwa kuwa hofu ndio inayokatisha maisha yao.

Amesema kumekuwepo dhana yenye mitazamo tofauti juu ya kila anayefariki dunia kuelezwa  kuwa amekufa kwa ugonjwa huo jambo hilo linasababisha wananchi kujawa na hofu na wengi wao kupoteza maisha na kusisitiza kuwa wilaya hiyo ipo salama.

Hata hivyo Sabaya amewataka wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga kwa kujifukiza majani yaliyoletwa na Mungu na kufanywa dawa ya kuwaponya na kuepuka matumizi ya chanjo ambayo ni biashara ya mabeberu na si salama sana.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Dkt Irene Haule amesema Jengo hilo la huduma za kinywa na meno limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 82 fedha ambazo zimetokana na mapato ya ndani.

Hata hivyo amesema kumekuwepo na changamoto ya upungufu kwa watumishi katika idara ya afya wilayani humo hasa katika kitengo cha huduma ya kinywa na meno kwani kati ya watumishi 10 wanaohitajika kwa sasa kuna watumishi watatu tu jambo ambalo linaleta changamoto kubwa katika utoaji huduma ya kinywa na meno kwa ufanisi.

Jengo la kinywa na meno katika hospitali ya wilaya ya Hai limegharimu kiasi cha shilingi milioni 82 hadi kukamilika kwake likitegemewa kuleta mapinduzi makubwa kwenye huduma mbalimbali za kinywa na meno ambazo awalii hazikuweza kufanywa kwenye hospitali hiyo kwa sababu ya kukosa vifaa.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UCHAGUZI MKUU 2020 October 10, 2020
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UCHAGUZI MKUU 2020 October 10, 2020
  • TANGAZO LA USIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI MWAKA 2020 October 20, 2020
  • Vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo 2020 May 30, 2020
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Sintoo Ahimiza Nidhamu Watumishi Wananchi Ofiisi za Umma

    March 01, 2021
  • Madiwani Kushiriki Kutokomeza Rumbesa Wilaya ya Hai

    February 24, 2021
  • Serikali Kuwakamata Wasiodai na Wasiotoa Risiti za Biashara

    February 17, 2021
  • DCC Yaishauri Halmashauri ya Hai Kuimarisha Vyanzo vya Mapato

    February 16, 2021
  • Ona Yote

Video

Wilaya ya Hai Nafasi ya 4 Kitaifa Darasa la Saba 2020
Vidio Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Planrep
  • TANEPS
  • Mfumo wa Ajira za Afya
  • Blog ya Wilaya
  • Fomu ya Maombi ya Likizo
  • Fomu ya OPRAS - Walimu
  • Fomu ya OPRAS - Watumishi
  • Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba Shule za Wilaya ya Hai Mwaka 2020
  • Muundo wa Halmashauri

Viunganishi Vinavyohusiana

  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya serikali
  • TAMISEMI
  • Mfumo wa Bajeti
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri nje ya nchi

Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitongoji cha Bomani

    Anuani ya Posta: 27 Hai

    Simu: 0272758441

    Simu ya Mkononi: 0752195133

    Barua Pepe: ded@haidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai