Mwenge wa Uhuru umefika katika Hospitali ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya afya yenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi wa Hai.
Miradi hiyo, ambayo imegharimu jumla ya shilingi milioni 900 inajumuisha ujenzi wa jengo la famasi, maabara ya kisasa, upanuzi wa wodi ya wazazi, ujenzi wa wodi ya daraja la kwanza pamoja na njia maalumu ya kupitisha wagonjwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya hospitali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025, Ismail Ali Ussi, amesema miradi hiyo ni sehemu ya jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya kwa watanzania kwa kuhakikisha huduma zinapatikana kwa wakati, kwa ubora na kwa ukaribu zaidi na wananchi.
Wananchi wa wilaya ya Hai wamepokea miradi hiyo kwa furaha na shukrani, wakieleza kuwa huduma bora za afya zinakuwa karibu tofauti na awali.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai