Serikali mkaoni Kilimanjaro Wilayani Hai imefanikisha zoezi la kuwaapisha wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba pamoja na uzinduzi wa Ofisi za baraza hilo.
Akizindua baraza hilo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mei 4, 2023 Mhe. Nurdin Babu amesema kuwa, ufanyaji kazi kwa kufuata maadili kwa wajumbe wa baraza hilo utasaidia kukamilika kwa wakati mashauri mbalimbali ya wananchi yanayohusu ardhi na nyumba ambapo hapo awali wananchi wa wilaya ya Hai walikua wakitumia muda mrefu pamoja na gharama kubwa kusafiri hadi wilaya ya Moshi kufuatilia haki zao.
Babu ameongezea kwakusema kua uteuzi wa wajumbe hao umezingatia utumishi na uelewa thabiti wa watumishi hao kisheria na katika usuluhishi wa ardhi na nyumba katika jamii tofautitofauti zinazopatikana katika wilaya hio na kuwataka Wajumbe hao .
Kufanya kazi kwa ufanisi na kufuata sheria za ardhi na kuhakikisha kuwa wanatoa haki na usawa kwa kila mwananchi.
Vilevile amefafanua kuwa, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Dk. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kusogeza karibu huduma za usuluhishi kwa jamii jambo ambalo pia litasaidia kupunguza gharama kwa wananchi na kutafuta haki zao kwa urahisi na kwa muda mfupi zaidi.
Ameongeza: "Wajumbe mnaoapishwa leo hii mmepewa dhamani kubwa kuhakikisha kuwa mnatatua migogoro ya wananchi wote bila kujali itikadi zao, udini wala ukabila, kwani Serikali inatarajia mabadiliko makubwa ya kuondoa changamoto ya ardhi na nyumba katika maeneo yote nchini," Alisema Babu.
"Mwenyekiti pamoja na wajumbe wako mashauri yanapofika yatatuliwe kwa muda mfupi na kwa ‘haki’, haipendezi kurundika mashauri bila sababu za msingi,"alisisitiza Mkuu wa Mkoa.
Babu alisema kati ya asilimia 40% mpaka 60% ya mashauri yanayopokelewa katika ofisi za wakuu wa Wilaya na ofisi ya Mkuu wa Mkoa yanatokana na ardhi na nyumba. Hivyo uanzishwaji wa Baraza hilo utasaidia
kupunguza mrundikano wa mashauri katika ofisi za watendaji na badala yake watafanya kazi zingine za kusimamia shughuli za kimaendeleo kwa maslai ya umma.
Babu amesema hayo wakati alipokua akiwaapisha wajumbe hao (4) watakao husika na usuluhishi pamoja na utoaji haki Wilayani Hai katika baraza hilo wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai