HAI
Jamii imeatakiwa kuzingatia na kutunza usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kuepuka magonjwa yanayoambukiza kama vile kipindupindu.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka katika kikao cha madiwani alipokuwa akijibu swali la diwani John Lengai aliyetaka kujua ni lini wananchi wataacha kuzifanya green belt kuwa dampo.
”mazingira ya green belt yapo katika makazi ya watu hivyo wananchi wanapaswa kupewa elimu kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira ili kuijikinga na magonjwa lakini pia kutunza mazingira”.
Amesema kuwa ili kuepuka utupaji taka katika maeneo mbalimbali ,sharia kali zinatakiwa kutolewa ikiwa ni pamoja na faini pamoja na kuwakamata wale watakaobainika kutupa taka hizo.
” tutumie sheria za mji mdogo kutoa adhabu kwa watu wanaotupa taka katika maeneo ya green belt”.
Amewataka pia afisa mazingira na afisa misitu kukagua green belt ambazo zimefanywa dampo kutoa elimu kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na kuweka sheria kali ili kuzuia utupaji taka katika maeneo hayo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai