Baraza la Madiwani halmashauri ya wilaya ya Hai kwa pamoja wamekubaliana kuendelea kuwahamasisha wananchi wilayani humo kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti 23 2022.
Kauli hiyo ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Hai imetolewa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Edmund Rutaraka katika kikao cha baraza la Madiwani ambapo amesema kuwa ili kufanikisha zoezi hilo ni vyema madiwani kwa kushirikiana na serikali kuunganisha nguvu ya uhamasishaji pamoja ili kuleta tija katika zoezi hilo.
Rutaraka ambaye pia ni diwani wa kata ya Muungano amesema kuwa kama kutakuwa na ushirikiano thabiti wa watendaji katika zoezi hilo kwa kushirikiana na madiwani zoezi hilo litafanikiwa kama ilivyokuwa katika zoezi la anuani za makaazi.
Akizungumza katika kikao hicho mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga amewapongeza madiwani katika kushirikiana na wataalamu ambapo na kuhimiza kuwa ushirikiano huo unapaswa kuendelezwa ili kusaidia halmashauri hiyo kupiga hatua katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Ikumbukwe kuwa katika zoezi lililopita la anuani za makaazi halmashauri ya wilaya ya Hai iliongoza kwa Zaidi ya 100%.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai