Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Edmund Rutaraka wamefanya ziara ya kikazi katika jiji la Mwanza yenye lengo la kujifunza namna nzuri ya ukusanyaji wa mapato.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo jijini Mwanza, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Edmund Rutaraka ameeleza kuwa jumla ya Madiwani 24 na wakuu wa idara wapo jijini humo kujifunza namna jiji hilo linavyokusanya mapato.
"Lengo la ziara tumekuja kujifunza hasa namna wanavyokusanya mapato wenzetu wa jiji hili la Mwanza lakini pia kuangalia matumizi bora kwenye upande wa mazingira kwasababu tunaona wenyewe ni mabingwa sana hasa kwenye kuchakata taka ili kwenda kuboresha mazingira katika halmashauri yetu ya wilaya ya Hai"
"Lakini pia kwenye mapato hawa ni mabingwa pia wa mapato, wenyewe wana njia mbalimbali za ukusanyaji hasa kwenye (Service Levy) kodi ya huduma, hotel Levy (ushuru wa nyumba za kulala wageni) na maeneo mengine"
"Wenzetu hawa wana miradi mikubwa ambayo wameletewa na Serikali lakini mingine wanaifanya kwa mapato ya ndani, sasa katika ile wanayoifanya kwa mapato ya ndani, kwa uwezo wetu katika halmashauri yetu mapato ya ndani yanaweza yakaleta maendeleo mengine kwa wananchi wetu wa Hai, naamini katika kujifunza huku tutakwenda kuleta mabadiliko kwenye halmashauri yetu kwa ajili ya wananchi wetu"
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai