Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imepokea fedha zaidi ya Shilingi Bilioni 1.7 za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Fedha hizo ni zile zinazotokana na tozo, Uvico 19 na kutoka Serikali kuu ambazo zimetolewa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na zinakwenda kutekeleza shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja ujenzi wa zahanati.
Akizungumza leo katika kipindi cha Drive home kinachorushwa na Redio Boma Hai fm, mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Dioni Myinga ameeleza kuwa kati ya fedha hizo Halmashauri imetenga jumla ya sh. Mil 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Chekimaji huku Mil.400 zikitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Longoi ili kuboresha huduma za Afya kwa wananchi.
Myinga ameeleza kuwa kutokana na upungufu wa madarasa jumla ya Sh. Mil 860 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 43 kwenye shule za sekondari zilizopo katika kata 13 kati ya kata 17 za wilaya hiyo.
Amezitaja kata ambazo zinakwenda kunufaika na ujenzi wa madarasa hayo kuwa ni pamoja na kata ya Bomang’ombe, Bondeni, Kia, Machame Mashariki, Machame Narumu, Machame Uroki, Masama Kusini, Masama Magharibi, Masama Rundugai, Mnadani, Muungano, Romu, na Weruweru.
Aidha mkurugenzi huyo amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi na kuona umuhimu wa kupeleka fedha hizo katika kila wilaya kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai