Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Hai kimesema kuwa kitaendelea kushirikiana na jeshi la Polisi katika kutokomeza vitendo dhalimu vya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto na watu wengine.
Akizungumza na Redio Boma Hai fm baada ya kutembelea dawati la jinsia na watoto katika kituo cha polisi Bomang'ombe, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya Chama Cha Mapinduzi wilayani humo Happiness Eliufoo aliitaka jamii hususani wanaume kupaza sauti ikiwa ni pamoja na kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti huyo ambaye aliambatana na Katibu wa CCM wilaya hiyo Ally Balloh pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa, kamati ya utekelezaji na madiwani wa viti maalum, alieleza kuwa wamepokea malalamiko ya ucheleweshwaji wa kesi mahakamani hali inayopelekea fedhea kwa wahanga wa ukatili.
Eliufoo ambaye ni askari Polisi mstaafu na amewahi kufanya kazi dawati la jinsia na watoto wilaya hiyo alipongeza jeshi la polisi wilayani humo na kuwataka kuongeza watendaji kwenye kitengo cha dawati hilo ili kuongeza nguvu ya kukabiliana na vitendo vya ukatili.
Akitoa taarifa juu ya kesi zinazoripotiwa dawati hilo, mkuu wa Polisi wilaya ya Hai Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Juma Majatta ameeleza kuwa kwa mwaka 2022 ziliripotiwa kesi 117, ambapo kesi 50 zinaendelea huku kesi 34 zikipata matokeo
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai