Diwani wa kata ya Masama kusini Cedric Pangani amemtembelea mkazi wa kijiji cha mkombozi Bi Farihia Kweka ili kumjulia hali na kutoa pole kufuatia nyumba yake kuungua moto.
Pangani amesema kuwa baada ya tukio la kuungua moto nyumba hiyo, mkazi huyo amepata hasara ya kuunguliwa na mifugo yake ambayo ni ng'ombe wawili na mbuzi wanane.
Pangani ameewaeleza waandishi wa habari kuwa chanzo cha moto huo ni jiko lilikuwa linawaka baada ya watoto kuliacha ndani likiwa linawaka.
Pangani amepongeza juhudi za majirani waliojitokeza nakushirikiana katika kuuzima moto huo ambao kama usingedhibitiwa ungeteketeza nyumba nzima.
Tukio hilo la ajali ya moto limetokea January 27, 2021 katika makazi ya Bi. Farihia Kweka wa kijiji cha Mkombozi kilichopo kata hiyo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 27 Hai
Simu: 0272758441
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai