Diwani wa kata ya Bomang'ombe Evod Njau ameahidi kushughulikia changamoto zinazowakabili watu wenye mahitaji maalumu kwenye kata yake ikiwemo kuwapatia wazee bima za afya.
Njau ametoa ahadi hiyo alipowahutubia wananchi wa kitongoji cha Uzunguni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa miguu kwenye kitongoji hicho wenye lengo la kuwashukuru kwa kukichagua Chama cha Mapinduzi kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.
Pamoja na kushughulikia changamoto hizo, Njau ameahidi kushughulikia na kupatia ufumbuzi changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana wa eneo hilo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Uzunguni Underson Somi amewataka wananchi kuwa na kawaida ya kuhudhuria mikutano inayoitishwa na viongozi ili kupata nafasi ya kuzielekeza kwa viongozi hao changamoto zinazowakabili.
Diwani huyo anaendelea kufanya mikutano na wananchi wa vijiji na vitongoji vilivyopo kwenye kata yake ikiwa ni kupata nafasi ya kujadiliana utatuzi wa changamoto zilizopo kwenye jamii.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai