Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Bomang’ombe ulio katika Halmashauri hiyo kuwaandaa wananchi kuwaelimisha kuhusu namna ya kuboresha mji huo.
Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha watumishi wa makao makuu ya halmashauri Sintoo amesema ili wananchi waweze kupokea maboresho hayo ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira ni llazima wapatiwe elimu ya kutosha.
“Tuwape wananchi elimu ya kutosha kuhusu utunzaji wa mazingira, uhifadhi wa taka pamoja na masuala ya mazao gani yanaruhusiwa na yanayokatazwa kulima ndani ya maeneo ya mji mdogo” Amesema Sintoo.
Amewataka kutafuta eneo litakalotumika kwa ajili ya makaburi huku akiwakumbusha kuzingatia kugawa maeneo hayo kwa ajili ya maziko ya jamii kulingana na imani zao.
Aidha amewata watumishi kuendelea kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wanaohudumiwa kwenye ofisi za halmashauri wapate huduma bora.
Akiwasilisha taarifa ya mipango ya kuimarisha mji mdogo wa Hai; Mtendaji Mkuu wa Mji huo Noel Nnko amemtaarifu Mkurugenzi kuwa mamlaka itasimamia katazo la kilimo cha mazao yenye urefu wa kama mahindi lakini wananchi wanaweza kulima maharage na mazao yanayofanana nayo.
Amesema kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo imeanza kusimamia sharia za mazingira ikiwemo kutoa adhabu kwa wanaotupa hovyo taka pamoja na wafugaji wanaoachia mifugo yao kuzurura na aina zote za uharibifu wa mazingira.
Kikao cha wiki hii kiliongozwa na ajenda ya mafanikio ya serikali katika wilaya ya Hai kwa miaka ya 2015 hadi 2019 ambapo Afisa Mipango wa Halmashauri Herick Marisham aliwasilisha taarifa iliyoandaliwa na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji ikionesha miradi iliyotekelezwa kwa fedha kutoka serikali kuu pamoja na ile iliyotekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za Halmashauri kupitia idara na vitengo vya halmashauri.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai