Mweenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Hai Edmund Rutaraka amewapongeza wahudumu wa Afya Msingi,watendaji wa vijiji na Kata Kwa kuwezesha Wilaya y Hai kufanya vizuri katika zoezi la usafi wa Mazingira na Unawaji wa Mikono.
Rutaraka ametoa pongezi hizo wakati wa kikao kazi kilichofanyika Kwa kuwasirikisha wahudumu Wa afya Msingi, Watendaji wa Vijiji na Kata.
Awali akimkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri,Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Hai Dkt Itikija Msuya amesema Wilaya ya Hai imekuwa ya kwanza kwa usafi wa mazingira na unawaji wa mikono Kwa Mkoa wa Kilimanjaro Kwa kupata asilimia 98.
Dkt Msuya amesema Hai imefanya vizuri kutokana na wahudumu hao Kutoa elimu ya afya na usafi Kwa Jamii.
Dkt Msuya amewataka kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha kuwa wilaya inaendelea kufanya vizuri.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai