*Katika Kusherekea Siku ya Wanawake Duniani, Wilaya ya Hai Yatoa Mikopo ya Milioni 500 kwa Kina Mama*
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Wilaya ya Hai imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500 kwa kina mama ili kuwawezesha kiuchumi na kuleta maendeleo endelevu katika jamii.
Akizungumza katika kongamano maalum la maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Hassan Bomboko, amesisitiza umuhimu wa jamii kuachana na mila potofu zinazorudisha nyuma maendeleo ya wanawake. Amehimiza wazazi kuhakikisha watoto wa kike na wa kiume wanapata fursa sawa katika elimu, akisisitiza kuwa elimu ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa.
"Ikiwa wazazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wasingempa fursa ya elimu, leo taifa lisingenufaika na uongozi wake mahiri, maono thabiti na dhamira yake madhubuti ya kuwaletea wananchi maendeleo," amesema Bomboko.
Ameongeza kuwa uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ni hatua muhimu katika kujenga jamii yenye usawa, na hivyo Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa kina mama kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya nchi.
Kongamano hilo limeleta hamasa kubwa kwa wanawake wa Wilaya ya Hai, wengi wakielezea matumaini yao kuwa mikopo hiyo itawasaidia kukuza biashara na kuboresha maisha yao.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai