Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Hai waamemchagua diwani wa kata ya Muungano Edmundi Rutaraka kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai huku diwani Swalehe Kombo wa kata ya Romu akichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Mapema hii leo madiwani 24 walikula kiapo cha maadili na kuwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Hai na mara baada ya kukamilika kwa kiapo hicho ndipo walipofanya uchaguzi wa mwenyekiti pamoja na makamu mwenyekiti wa halmashauri.
Awali katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe ambaye pia ni diwani katika baraza hilo ambaye amesema kuwa mara baada ya kuapishwa kuwa mbunge wa jimbo la Hai alifanya ziara katika kata zote za wilaya ya Hai na changamoto kubwa zinazolikabili jimbo lake ni pamoja na zile zinazotokana na vyama vya ushirika pamoja na masuala ya ulevi.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa pia na mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole sabaya pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama, Sabaya amewataka madiwani walioapishwa kufanya kazi kwa misingi ya haki na uadilifu na kutambua kuwa wamepewa dhamana kubwa ya kuwatumikia wananchi na hivyo waitumie vyema fursa hiyo ili kutatua changamoto zilizopo katika jamii.
Jumla ya madiwani waliokula kiapo hii leo ni mdaiwani 24, kati yao madiwani 17 wakiwa ni wakuchaguliwa na 7 wakiwa ni wale wa viti maalumu hii ikiwa ni kutokana na uchaguzi mkuu uliofanyika octoba 28 mwaka huu ambapo chama cha mapinduzi kilishinda kata zote katika wilaya ya Hai.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai