Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa Madarasa ifikapo tarehe 15.12.2021
Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo Nov 16 2021 alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kuwa hakutakuwa na uchaguzi wa awamu pili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza na kuziagiza Halmashauri zote kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa madarasa kwa wakati ili wanafunzi wote wanaofaulu kujiunga na kidato cha kwanza waanze kusoma kwa wakati mmoja.
Amesema fedha za UVIKO 19 zimetolewa kwa lengo la kuendeleza miradi ya maendeleo kwenye sekta ya Afya, na Elimu hivyo Viongozi wa Mikoa yote nchini wanawajibu wa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ukamilishaji wa ujenzi wa miradi kwa wakati.
Aidha Waziri Ummy ametoa maelekezo kwa Halmashauri zote kutumia mapaa yenye migongo miwili ili kupunguza gharama za ujenzi na kuwataka kutumia tarazo au sakafu za kawaida kwa kuwa vigae vinavyowekwa kwenye ujenzi wa madarasa vipo chini ya viwango.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Edmund Rutaraka amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa jitihada zake za kuboresha miundombinu ya shule ambapo pia amemuomba Waziri kuwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili na uzio katika shule ya Sekondari ya Hai.
Halmashauri ya Wilaya ya Hai imepata kiasi cha shilingi milioni 860 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 43 vya madarasa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai