Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo ameshauri wataalamu wa afya kuona namna ya kuongeza huduma za madaktari bingwa katika Hospitali ya Wilaya ya Hai ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi.
“Hizi huduma ni adimu huku kwetu na wapo watu wengi wanaozihitaji; na muda wa siku nne hautoshi kumaliza watu wote. Nimesikia huduma hii ya kliniki tembezi itatufikia tena baada ya miezi minne; niombe kama itawezekana iwe inafanyika kila baada ya miezi mitatu”. Ameongeza Sintoo.
Amewataka kuwa na huduma za kibingwa walau kwenye kila robo mwaka yaani kila baada ya miezi mitatu ili kuweza kuwahudumia wagonjwa waliokosa huduma kutokana na wingi wa wananchi wanaohitaji huduma hizo.
Awali akijibu swali la mwananchi Swalehe Mshana aliyetaka kuongezwa kwa huduma hizo hadi kwenye ngazi ya vituo vya afya; Mganga Mkuu wa Wilaya ya Hai Dkt. Irine Haule amesema kuwa huduma za madaktari bingwa zimepangwa kufanyika kila baada ya miezi minne ikiwa ni jitihada za kufikisha huduma hizo kwenye wilaya zote za Mkoa wa Kilimanjaro.
Huduma ya kliniki tembezi inafanyika katika hospitali ya Wilaya ya Hai kwa siku nne kuanzia tarehe 25/02/2020 hadi 28/02/2020 ikihusisha madaktari bingwa kutoka hospitali ya rufaa ya Mawezi, KCMC na madaktari bingwa kutoka hospitali ya wilaya ya Hai wakihudumia wagonjwa wa macho, pua, koo, sikio, mifupa, magonjwa ya wanawake na watoto huku kukifanyika upasuaji mbalimbali.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai