Diwani wa kata ya Masama Kusini Cedrick Pangani ameahidi kuchangia mifuko 10 ya saruji katika ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ambao umeanza katika Kijiji cha Kwasadala unaotarajiwa kugharimu jumla ya shilingi milioni 605 hadi kukamilika kwake.
Pangani ametoa ahadi hiyo alipozungumza na wananchi wa eneo la hilo katika mkutano wa hadhara kwa lengo la kuweka mikakati ya kuanza rasmi ujenzi wa shule hiyo.
"Mimi binafsi naahidi mifuko 10 ya cement, lakini huwa nna tabia nikilibeba jambo nalibeba kama la kwangu kwahiyo tutashirikiana na nimeshampigia injinia atuletee ramani"
"Kwahiyo kuanzia leo tujifungeni mkanda tusisikiliza la mtu, sisi tunachoona na tunachofikiria kitokee kwenye maisha yetu, wote tuongee lugha moja tutengenezeni hii shule na hii thawabu tutaikuta huko juu haitakaa ifutike.
Kwa upande wao wananchi wa kata hiyo wameeleza kuwa wamepitia adha ya kukosekana kwa shule ya sekondari katika eneo hilo hali iliyopelekea wanafunzi kutembea umbali mrefu na ndiyo maana wameamua kuungana na diwani wa kata hiyo kuanza ujenzi mara moja.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai