Katibu Tawala Wilaya ya Hai Upendo Wella amewataka wananchi wa kata za Kia na Masama Rundugai kuchua tahadhari ya mafuriko kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.
Ametoa wito huo leo April 03,2023 wakati akizungumza katika daraja la mto Biriri Kwa wasomali wilayani Hai baada ya maji kujaa na kufunga barabara ya kuu ya Moshi-Arusha hali iliyopelekea magari kusimama kwa masaa mawili.
Wella amesema ni vema wananchi wakachukua tahadhari kwa kuwa mvua zinazoendelea zinaweza kuleta madhara endapo zitanyesha kwa wingi na kwa kuwa wakati mwingine maeneo hayo huathirika na mvua ambazo zimenyesha katika ukanda wa juu.
“Leo majira ya kuanzia majira ya saa tatu kuelekea saa nne ndipo tulipata taarifa kuwa kwenye eneo letu la daraja la mto Biriri ambapo maji yalikuwa yamekuja mengi sana kutoka ukanda wa juu kitu ambacho tumejaribu kufanya mawasiliano na wenzetu wa wilaya ya jirani (Siha) ndipo tukaambiwa ni kweli mvua imenyesha katika wilaya ya Siha”
“Kwa hiyo maji hayo yale ambayo yametokana na mvua ndiyo ambayo yameporomoka na kushuka ukanda huu wa chini na kupelekea kupita juu ya daraja lile na watu kushindwa kuvuka kwa muda huo kwa sababu maji yalikuwa ni mengi sana ambapo tukio hilo lilichukua takribani masaa mawili na tulifanya mawasiliano na wenzetu wa TANROAD mkoa wakafika kukagua na kueleza kuwa daraja liko salama”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai