KATIBU tawala wilaya ya hai ndg SOSPETER MAGONERA amefungua rasmi maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyozinduliwa katika Mahakama ya mwanzo iliyopo wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Maadhimisho hayo ambayo yanahusisha utoaji wa elimu ya kisheria kwa wananchi bila malipo, yataendelea mpaka tarehe 3 ya mwezi wa 2 ikiwa ndiyo siku ya kilele cha maadhimisho hayo
Hata hivyo MAGONERA ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo amewataka wananchi wa wilaya ya hai kujitokeza kwa wingi katika wiki ya sheria kutembelea Mahakama zilizopo karibu ili kupata elimu ya kisheria.
Pamoja na hayo amesema ni muhimu kwa kila mwananchi kuitambua nafasi yake kwa kuhakikisha anapata huduma ndani ya siku zilizotajwa kwani kwa kufanya hivyo itawajengea uelewa mzuri kupitia elimu hiyo
Kwa upande mwingine amezungumzia dhana kamili ya kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya wiki ya sheria ambapo amesema kauli mbiu inatoa hamasa kwa taasisi zote zinazosimamia haki kwa kuzingatia dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2050
Kwa upande wake hakimu mfawidhi mahakama ya wilaya ya Haii bi Julieth Maole amezungumzia namna ambavyo kesi kwa mwaka 2024 zilivyopungua hadi kufikia 104 ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wakifunga mwaka na kesi 400 mpaka 600
Hata hivyo amesema lengo lao kwa mwaka 2025 ni kuhakikisha kesi za uhalifu zinapungua Zaidi au kumalizika kabisa huku akisisitiza yakwamba jambo hilo linawezekana.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai