Wazazi na walezi wametakiwa kuwaombea Watoto wao ili waweze kufanya vizuri kwenye mtihani wa darasa la saba unaotarajiwa kufanyika kuanzia siku ya kesho tarehe 5 na tarehe 6 mwezi huu.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa elimu wa shule za msingi wilaya ya Hai Mwalim Sinyi Kitimbi Leo tarehe 04, Oktoba kwenye mahojiano maalumu ambapo amesema kuwa kwa sasa maandalizi yanaendelea na mtihani utafanyika kwa siku mbili na wilaya ya hii kwa mwaka huu 2022 ina watahiniwa 5883 ambapo wanapatikana kwa jumla ya shule 129.
“Ndani ya shule hizo kuna jumla ya mikondo 279, ndani ya hizo tumegawa vituo teule vya kuhifadhia mitihani vituo 26 ni vya msafara,na vituo vya kulazia mitihani 19 ambavyo ni vituo teule, kwahiyo mpaka sasahivi kwa ujumla maandalizi yapo tayari na wasimamizi wameanza kulipwa pia na usafiri wa kuwapeleka wasimamizi maeneo yao ya kazi yapo tayari pia”
Ameongeza kuwa wazazi na walezi wanapaswa kuwa waangalifu kwa kuwakataza Watoto wao kufanya udanganyifu kwa namna yoyote ile iwe kufanya ili washinde au washindwe, na kukataa udanganyifu hata kwa kutumwa na mtu yeyote.
Lakini pia amewaasa wasimamizi kuwa waaadilifu na waaminifu wakiwa kwenye majukumu yao ya kusimamia mitihani na kuepusha udanyanyifu wowote kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao.
Mtihani wa Taifa wa darasa la saba unafanyika nchini kila mwaka Kwa lengo la kupima uelewa wa wanafunzi kabla ya kuanza masomo ya sekondari kidato cha kwanza.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai