Umoja wa Machifu hapa nchini unakusudia kuyarejesha masalia ya binadamu ikiwemo mafuvu ya kichwa zaidi ya 32 yaliyopo Ujerumani yaliyochukuliwa wakati wa utawala wa wajerumani lengo likiwa ni kuyaenzi na kuongeza pato la taifa kupitia utalii.
Katika tamasha la utamaduni lililofanyika Januari mwaka huu, Machifu hao walimuomba Rais Samia ambaye Pia ni Chifu mkuu wa Machifu Tanzania, kurejeshwa masalia hayo ambapo Rais alizielekeza wizara zinazohusika kuchukua hatua stahiki ili kurejesha masalia hayo.
Katibu wa Machifu mkoa wa Kilimanjaro Joseph Msele akizungumza kwenye maonyesho ya marejesho hayo yaliyofanyika Septemba 10, 2022 Kyalia Machame wilayani Hai, anasema kwamba "Tumepata taarifa nzuri kutoka kwa watanzania wanaoishi Ujerumani ambao nao wamekuwa na harakati kama hizi, ambapo katika juhudi hizo chini ya kikundi cha Berlin Post-Colonial, tayari wamepata idhini ya awali kwamba hivyo vitu vinaweza kurudishwa"
"Kwa taarifa ni kwamba Berlin pekee kuna mafuvu ya binadamu zaidi ya 22 na kwa mji mwingine ulioko mpakani mwa Ufaransa kuna mafuvu zaidi ya 32 na haya ni yale ambayo yanahusu ukanda wa kaskazini kwa maana yana lebo ya Chaga, lakini vitu vingine ambavyo ni vya jadi vipo zaidi ya 300 na kwa Tanzania nzima ni zaidi ya 2000"
Diwani wa kata ya Machame Kaskazini Judica Mushi akizungumza katika maonesho hayo ameleeza kuwa hakuna haja mafuvu hayo kuendelea kukaa Ujerumani, ni wakati sasa wa kuyarudisha ili watanzania waweze kuyaenzi kwa lengo la kuleta kumbukumbu nzuri na kitega uchumi katika masuala ya utalii.
Akiwasilisha salam za mkuu wa wilaya ya Hai Juma Irando, Afisa tarafa ya Machame Said Izina amewapongeza viongozi walioandaa maonesho hayo ya kuenzi utamaduni kwani husaidia huonyesha ni wapi watanzania wametoka na kipi wanapaswa kupambania kiujumla.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai