Mbunge wa jimbo la Hai Mhe. Saashisha Mafuwe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kulipatia jimbo hilo fedha nyingi zinazopelekea uwepo wa miradi mikubwa ya kimaendeleo katika wilaya hiyo kwa wakati mmoja.
Saashisha ameyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa jimboni humo na kuzungumza na wananchi huku akiwataka wakandarasi wanaohusika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa weledi ili wananchi wafaidi matunda ya Serikali ya awamu ya sita.
“Kwakweli tunatakiwa kumpongeza sana mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo analitendea jimbo la Hai hivi sasa kuna barabara nne ujenzi unaendelea kwa kiwango cha lami ile kero ya muda mrefu ya maji inamalizika maji yashaanza kupampiwa hali inayopelekea upatikanaji wake kuongezeka yapo mengi yanayofanyika nikiyazungumza siwezi kuyamaliza ikiwemo hilo la ujenzi katika hospital yetu ya wilaya ambapo shilingi bilioni 1.3 zimepelekwapale na mkandarasi anaendelea na kazi”
Akifafanua zaidi Saashisha ameeleza kuwa fedha hizo zitasaidia ujenzi wa majengo manne katika hospital hiyo ambapo yanatarajiwa kuboresha huduma za afya kwa wagonjwa na kuongeza kuwa katika fedha hizo milioni 300 zitanunua vifaa tiba na dawa huku milioni 50 ikienda kwenye zahanati na kutaja kuwa fedha nyingine zilizobaki ambazo ni milioni 900 ndizo zitakazo husika na ujenzi katika hospital ya wilaya huku akibainisha kuwa upatikanaji wa dawa katika hospital ya wilaya umeboreka hadi kufikia asilimia 96 .
“Nawataka wakandarasi kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na haraka ili miradi hii mikubwa itimie kwa wakati kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Hai namshukuru sana waziri wa afya na namna anavyosikia maoni ya wabunge hili jambo niliiomba serikali nikiwa bungeni kufanya matengenezo ya hospital yetu ya wilaya na kutuongezea majengo na leo limeshanyika tunachomuahidi mheshimiwa Rais ni kwamba tutaendelea kumpenda na tutahakikisha miradi yote inayokuja wilaya ya Hai tunaisimamia ili Ile shauku yake , maengo na matajio yanatimia ikiwa ni pamoja na kuakikisha thamani ya fedha inaonekana kwenye miradi hiyo”
Akizingumza katika ziara hiyo Diwani wa kata ya Bomang’ombe Evod Njau amempongeza mbunge huyo kwa namna anavyopambana kuakikisha fedha za maendeleo zinafika katika jimbo hilo na kuongeza kuwa ushirikiano mkubwa baina ya madiwani ofisi ya mkuu wa wilaya mkurugenzi na mwenyekiti wa halmashauri unafanya fedha hizo zitumike kwa weledi kwani ufuatiliaji unafanywa mara kwa mara kuhakikisha zinanufaisha wananchi ambao ndio walengwa.
Kwa upande wake katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Hai Mudi Msalu amesema fedha za uboreshaji wa hospitali hiyo ni matokeo ya maamuzi sahihi ya wananchi wa wilaya hiyo kukiamini Chama Cha Mapinduzi na kukipa nafasi ya kuongoza jimbo hilo kuanzia nafasi za wenyeviti wa vijiji na vitongoji madiwani mbunge na rais hivyo wana kila sababu ya kufurahia matunda ya kura zao kupitia maendeleo makubwa yanayofanyika jimboni humo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai