Katika kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru viongozi kwa kushirikiana na wananchi wamefanya usafi katika soko la Mailisita lililopo Kata ya Mnadani kuelekea Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku wananchi kuharibu mazingira kwa kutupa taka hovyo.
Akizungumza mara baada ya zoezi la usafi Katibu Tawala wilaya ya Hai Upendo Wella amesema"Viongozi wamekuja kufanya usafi eneo hili ili kuwapa fundisho, haipendezi watendaji watoke Wilayani kuja kufanya usafi kwenye maeneo yenu wenyewe mliyoyachafua na eneo hili ni marufuku taka kuwekwa tena uongozi wa Kijiji utapaswa kuwajibika katika hili"
"Natoa wiki moja kwa uongozi wa Kijiji Shiri Njoro kuwasilisha mpango kazi wa namna ya kuweka mazingira haya safi kwa kuwa na dampo sehemu nyingine tofauti na hili lililopo karibubna ofisi za serikali na makazi ya watu,ikiwa ni pamoja na kuwaonesha wafanyabiashara eneo maalum la kuweka taka zinazo zalishwa"
"Siku hizi takataka zimekuwa ni fursa kwani zina chakatwa na kutengeneza bidhaa nyingine kama mkaa,hivyo mipango inahitajika kuwekwa ili kuendea fursa za namna kama hiyo na watu wachangamkie fursa hiyo" amesema Upendo Wella
Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga amesema kuwa "Ni marufuku kwa mwenyeji wa wilaya yetu ya Hai au mgeni kutupa taka hovyo kwenye maeneo naagiza watendaji wangu kusimamia hilo na kilele cha siku ya Uhuru nitapitia kwenye maeneo kufanya ukaguzi" Dionis Myinga
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai